Watu wawili akiwano Meneja wa duka la kubadilisha fedha za kigeni la jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa kuuza dawa za kulevya nchini na kumeweka mwenzao rehani ughaibuni.
Naibu Kamshna wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dra es Salaam, Simon Sirro, aliwatawaja watuhumiwa hao wote wakazi wa jijini Dar es Salaam kuwa ni Nassoro Suleiman (35), ambaye ni Meneja wa Dula la Kubadilisha Fedha Kigeni la Tungwe lililoko katika jengo la IPS na mfanyabiashara Mohamed Omari (37).
Naibu Kamishna Sirro alifafanua kuwa Omari anatuhumiwa kuhusika na kusafirisha dawa na usafirishaji binadamu pamoja na kumuweka rehani Mwinyi Mgobanya, nchini Pakistan.
"Alimuweka bondi Mgobanya ili kuchukua dawa za kulevya kwa mali kauli huko Pakistan," alisisitiza Kamanda Sirro.
Alisema Suleiman anatuhumiwa kwa kushirikiana na genge la wauzaji dawa za kulevya na kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha kwa njia ya zisizo rasmi.
Tangu mwaka 2014, jumla ya kilo 305 za heroin na kilo 39 za cocaine, zilikamatwa na watuhumiwa 14,501 walikamatwa kati yao Watanzania wakiwa 14,467.
Kamanda Sirro alisema ongezeko la uhalifu wa dawa za kulevya kimataifa ni kukua kwa mitandao na magenge katika nchi za Kiarabu.
Wakati huo huo, Kamanda Sirro amesema jumla ya Sh. milioni 722 zimekuswanywa kutokana na operesheni ya kuhakikisha madereva wanafuata sheria za usalama barabarani kuanzia Januari 2, mwaka huu.
Na katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amewataka Wahariri wa gazeti la Mawio kujisalimisha Polisi kabla ya jeshi lake halijaenda kuwakamata ili kujibu tuhuma za uchochezi kupitia gazeti hilo.
Katika tukio lingine, watu sita wametiwa mbaroni kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa hao ni Abdallah Juma, Victor Gabriel, Prosper Gervas, Agasese Mala, Mohamed Abdul, wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment