Tuesday 12 January 2016

MICHEZO: MESSI MCHEZAJI BORA WA DUNIA ATWAA BALLON D'Or 2015


Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia 2015 Leon Messi katikati
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or award ) kwa mwaka 2015 huku akiwashinda wapinzani wake wa karibu Christian Ronaldo na Neymar, ikiwa ni mara ya tano kutwaa tuzo hiyo.

Messi, 28, amepata asilimia 41.33 ya kura zote zilizopigwa akifuatiwa na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo mwenye asilimia 27.7 wakati Neymar wa Barcelona akiambulia asilimia 7.86 ya kura zote.

Messi na Ronaldo kwa pamoja wameshinda tuzo hiyo mara nane.



Via-Kigomaonline.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!