Monday 11 January 2016

MBWANA SAMATTA AMTEMBELEA SHEIKH MKUU KATIKA OFISI ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM


Leo Tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.




Mufti Mkuu mbali na kumpatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko aendako Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi. 





Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye. 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!