Monday 25 January 2016

JOCKTAN MALULI, DANIEL MSIRIKALE WAIBUKA WASHINDI KATIKA SHINDANO LA BONGO STYLE



Mshindi wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke(aliyeshika cheti) akiwa katika picha ya pamoja na  waratibu wa shindano hilo kuanzia kushoto ni  Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora na Stanley Kamana.


Mshindi wa kipengele cha The Best Photographer, Daniel Msirikale (mwenye miwani) akipokea tuzo yake.
Mlezi wa FASDO, Reuben Nabora akitoa salamu kutoka kwa mwasisi wa FASDO, Lilian Nabora aliyeko Ubelgiji.
Mratibu wa FASDO nchini, Joyce Msigwa  akitoa muhtasari wa shindano la Bongo Style.
Mshereheshaji, Mario Mpingirwa akifafanua jambo.
Mtumbuizaji wa ngoma za asili akionesha uwezo wake wa kuchezea nyoka.
 Baadhi ya viongozi wa wa FASDO wakifuatilia shindano hilo.
Majaji wa ubunifu mitindo wakitathmini kazi za washiriki wao.
Majaji wa upande wa wapiga picha wakitazama kazi za washiriki wao.  
Mshindi wa ubunifu mitindo, Jocktan Maluli 
  akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wanaoonesha mavazi yake.
 Wanamitindo wakionesha mavazi yaliyobuniwa na washiriki.
 Washiriki wa ubunifu wa mitindo wakitambulishwa mbele za watazamaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Entango, Emma Kawawa akitoa salamu zake na kuendesha harambee kwa ajili ya FASDO.
Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Chande akizungumza jambo.
Mwenyekiti wa FASDO, Stanley Kamana akiongea jambo.
 Mshindi wa kipengele cha Best Personality of The Year, Shahbaaz S. Yusuf akipokea tuzo kutoka kwa mlezi wa FASDO, Reuben Nabora.
 Mshindi wa Peoples Choice Awards for Fashion Designer, Winfrida Touwa akipokea tuzo yake.
Mshindi wa Peoples Choice Awards for Photograph, Rasheed Hamis akipokea tuzo.
 Msanii Alvin Dullah 'DY' akitumbuiza baadhi ya nyimbo zake.
 Baadhi ya washiriki wakichukua vyeti vya ushiriki wa shindano hilo.
 Baadhi ya watu wakijifotoa.
 Baadhi ya wadau wakiongozwa na Mzee Nabora wakizitazama picha za washiriki.
Umati wa watu waliohudhuria fainali hizo wakifutatilia shindano hilo kwa umakini.
(Picha na Fredy Njeje)

WASHIRIKI wa shindano la Bongo Style linaloratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya FASDO, Jocktan Cosmas Maluli  (25) na Daniel Msirikale (24) wameibuka kidedea kwa kujinyakulia tuzo za shindano hilo katika fainali iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.

Shindano hilo lililoanzishwa mtandaoni mwezi Septemba mwaka 2015, lilijumuisha washiriki wapatao mia tatu wenye vipaji vya upigaji picha na ubunifu wa mitindo huku washiriki kumi pekee wakiingia kwenye fainali baada ya michujo mbalimbali kabla ya washiriki hao wawili wakishinda tuzo hizo.

Washiriki hao walishinda kutokana na kura za majaji waliobobea katika fani hizo ambapo kwa upande wa picha majaji hao walikuwa ni: Sameer Kermalli, Hanif Abdulrasul, Idd John na Angela Kilusungu huku kwenye ubunifu wa mavazi majaji hao wakiwa ni: Martin Kadinda, Rio Paul, Zamda George na Comfort Badaru.

Jocktan Maluli ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Fashion Designer 2015 na Daniel Msirikale aliyeshinda katika kipengele cha Best Photographer 2015, wote pamoja wamepokea kitita cha dola 500 kila mmoja huku wakipata nafasi ya kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuonesha ubunifu wao katika maonesho ya Africa Firm Festival Belgium kuonesha kazi zao pamoja na washiriki 18 walioshiriki shindano hilo, yatakayofanyika hivi karibuni nchini humo.

Aidha washindi wa vipengele vingine ni: Shahbaaz  Yusuf aliyeshinda kipengele cha Best Personality of the Year 2015, Winfrida Touwa aliyeshinda katika kipengele cha Peoples Choice Award for Fashion Designers na Rasheed Rasheed aliyeshinda kipengele cha Peoples Choice Awards for Photograph.

Fainali hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa na wadau mbalimbali wa kazi za sanaa na kupambwa na burudani mbalimbali kama vile nyimbo za asili, muziki na maonesho ya mavazi na kazi za sanaa kutoka kwa washiriki hao.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!