Mwenyekiti wa kikao cha Bunge Andrew Chenge ameahirisha kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea mjini Dodoma.
Chenge amefikia uamuzi huo kutokana na kuibuka kwa mjadala mkali kutoka kwa Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee kulitaka bunge liahirishe kikao ili wabunge wajadili hoja ya waziri Nape Nnauye.
Hoja ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye Bunge ni kwamba shirika la utangazaji la Taifa TBC halitarusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge (live) bali kutakuwa na kipindi maalumu kitakachoitwa Leo katika Bunge.
Hoja hiyo imezua mjadala mkali na kumfanya mwenyekiti wa Bunge kuahirisha kikao cha bunge kwa muda wa lisaa limoja ili kikao cha kamati ya bunge kikakae na baadae waje na njia muafaka ya kuweza kutatua jambo hilo.
No comments:
Post a Comment