Tuesday, 12 January 2016

BANK ZA MLIMANI CITY ZAINGIA KATIKA KASHFA NZITO ZA KUTOA SIRI ZA WATEJA KWA MAJAMBAZI

UJAMBAZI MLIMANI CITY
Wadau, habari za asubuhi;
Hapa maeneo yetu kuna msiba umetokea. Marehemu ameuwawa na majambazi. Alichukua fedha (milioni 10) kutoka Benki mojawapo hapa Mlimani City na kuanza safari ya kuelekea huko Salasala ambako alikuwa na shughuli ya ujenzi inayoendelea. Majambazi walimfuata kwa nyuma, walimpita na kumzuia kwa mbele. Majambazi walimtaka atoe 10M aliyochukua Benki kabla ya kumpiga risasi. Walikuwa wanafahamu kiasi halisi kilichochukuliwa!




Siku kama 5 kabla ya tukio hili, tukio lingine lilitokea eneo la Bamaga (mkabala na Hongera bar). Mtu na mke wake walichukua fedha toka benki hapo Mlimani City (13m). Majambazi walimfuata kuanzia hapo Mlimani city hadi huko Bamaga na kumtaka awape fedha. Kumbe alikuwa amezitenganisha; aliwapa laki 5 lakini walipatwa na hasira na kuhoji fedha nyingine ilikuwa wapi. Walimpiga risasi begani. Mke wake akawaongezea laki 1; naye alijeruhiwa kwa risasi wakidai "tunataka milioni 13 zote". Pona yao ni kuwa fedha walikuwa wameificha kwenye booth. Baada ya kuona muda unapita majambazi wakaondoka. Na kwa bahati nzuri majeruhi walipona. Cha kushangaza ni kuwa majambazi hawakujifunika nyuso zao wala hawakuwa na wasiwasi wa kujificha hata kidogo.
Huko nyuma, jirani yetu mmoja (Mama-Joshua) alichukua milioni 4 hapo hapo Mlimani City. Baada ya kufika kwa Kakobe, majambazi walimpita na kumsimamisha baada ya kujifanya kuwa wanamjua. Baada ya kusimama walimtaka awape "awape mzigo aliochukua benki". Hivyo:
1. Mlimani city ni eneo hatari sana kwa ujambazi;
2. Inaelekea wafanyakazi wa Benki wanashirikiana na majambazi. Hivyo, kitendo cha wewe kwenda kuchukulia fedha ndani ya benki (bulk cash room) hakiwezi kuwa ni cha siri;
4. Epuka kuchukua fedha nyingi benki. Fanya malipo kupitia benki au njia nyingine mbadala;
4. Kama una ujenzi, ni hatari kuwa na kawaida kuwapelekea mafundi fedha kwenye site; tumia M-pesa, tigopesa, nk.
5. Kama umechukua fedha, usikubali kusimamishwa na mtu usiyemjua njiani isipokuwa kama wameku-block na huna jinsi ya kukwepa.
Mjulishe rafiki, ndugu na jamaa kuhusu changamoto hii ya kiusalama..
AS RECEIVED

HAYA NDO BAADHI YA MAONI YA RAIA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!