Wednesday 13 January 2016

ATHARI YA VYAKULA VYA KUKAANGA:

 


Uwepo wa wajasiriamali wadogo kila kona mitaani wakiuza vyakula vya kukaanga kwenye mafuta pekee kama vile chipsi,kuku,mayai,maandazi,chapati,bagia,kaimati,sambusa,nyama za mbuzi,n'gombe na nguruwe.





.Vyakula hivi hupatikana pia hotelini,mgahawani,baa nk sanjari na bugger,pizza,sausage nk na huambatana na chachandu'salad',mkorogo wa maziwa mayai'mayonaise'

 pamoja na chupa ya soda ambazo huwa na sukari nyingi.
.Ulaji wa vyakula hivi pasipo kufanya mazoezi mepesi wala kuushughulisha mwili wala kusogeza misuli na viungo vya mwili husababisha unene ulopitiliza,magonjwa ya moyo,kisukari,shinikizo la damu,magonjwa ya figo nk.Mara nyingi walaji wa vyakula hivi wengi huvisifia kuwa na utamu na vinahamasisha hamu ya kuvitumia pamoja na juice au soda bila kufahamu kwamba vyakula hivi vina kiasi kikubwa cha wanga,mafuta mengi,sukari na chumvi nyingi na kusababisha walaji wengi kuwa wanene na kupata maradhi yatokanayo na unene uliokithiri.Njia sahihi ni kupunguza ulaji na kufanya mazoezi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!