Friday 1 January 2016

ASANTENI SANA!

Wapendwa wadau  wa Sophiembeyu Blog, kwanza kabisa natoa shukrani zangu kwenu kwa kunipa mapenzi na faraja kubwa, mmekuwa ni familia yangu yapili kwa kushirikiana  nami  hadi mwisho wa  mwaka 2015.  kwa ujumla tangu nianze kublog
hamjanitupa


Sophiembeyu Blog inaahidi kuendeleza "libeneke" kwa kasi na nguvu mpya kabisa!  Napenda kutoa heshima zangu kwenu wadau wangu kwani hamkunitupa no matter what" kwa mahaba mlionionyesha wapendwa, naona sitaacha kublog, "MAHABA MAKUBWA SANA HAYA"nitakaza buti mpaka vidole vipinde, Na pia naomba msamaha kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine niliwakwaza, wakakwazika! Tusameheane.
 Sasa na nyie msisite kuniandikia kwa lolote! kama unashughuli yako harusi, Birthday, Habari Wachumba ... just name it! Mie nitaisukuma humu, bila wasiwasi ili mradi isiwe ya ugombanishi matusi,siasa zenye uchochezi, dini na vinginevyo. 
Mwaka wa 2016 na uwe  mwaka wa mafanikio, utulivu, amani upendo na  furaha na vicheko teeele!.

Haya kanyageni twende sasa! 2016 naije!!

HAPA KAZI TU!
Narudia tena Asanteni Saaana, halafu mjue mie nawapendaga tu yaani!!

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!