Vigogo wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) waliokamatwa katika sakata la upotevu wa makontena 349, leo wanatarajiwa kuanza kufikishwa mahakamani.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema idadi ya watuhumiwa imeongezeka kutoka 12 na kufikia 29 ambapo kati ya hao, 18 ni wa TRA.
Akihojiwa na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani, alisema idadi wa watuhumiwa imeongezeka ambapo juzi na jana waliwakamata watuhumiwa 17.
Alisema kati ya idadi hiyo, 13 wanatokea TRA na wanne wanatokea maeneo mengine.
Awali walikamatwa watuhumiwa 12 na wakiongezwa hao 17, wanafikia 29.
“Kama ilivyokuwa awali, majina ya watuhumiwa hao sitayataja kwa ajili ya upelelezi wetu unaoendelea,” alisema Kamanda Athumani.
“Inawezekana kesho (leo), tukaanza kuwapunguza baadhi yao kwa kuwapeleka mahakamani," alisema.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, serikali ya awamu tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, ilibaini ubadhirifu wa upotevu wa makontena 349 ambayo yameisababishia serikali Sh. bilioni 80 kutokana na kukwepa kodi
NIPASHE.
No comments:
Post a Comment