Wednesday, 9 December 2015
UNGANA NA MDAU ANNAPETER APEMA DESEMBA 12 2015 KATIKA MATEMBEZI YA HIARI KUUNGA MKONO WATOTO WENYE MATATIZO YA VICHWA NA MGONGO WAZI
Ndugu zangu wapendwa.Kwanza naomba nitangulize kuomba radhi kama picha hapo chini kama itawasumbua watu wengine ila ndio hali halisi.Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa sana na tatizo la watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi.
Hili tatizo linatokana na mama akiwa mjamzito kutopata vyakula vyenye vitamini za Folic Acid.Watoto hawa wana mahitaji mengi.Pale hospitali ya Taifa Muhimbili kuna wodi maalum kwa ajili ya watoto hawa.Mimi kama mmoja wa marafiki wa watoto hao nawaomba tujitokeza kuwaunga mkono ambapo Jumamosi Desemba 12 ,2015 Chama cha wazazi wenye watoto wa tatizo hilo(ASBATH)watafanya matembezi kutoka Kariakoo kuanzia saa tatu asubuhi na yataishia Muhimbili.Waweza kuja na chochote iwe nguo,vyakula kama mchele,unga,maziwa ya unga,mafuta ya kupikia,sukari,khanga na vinginevyo ili kuwapatia wazazi na watoto wanaolazwa hospitali hapo kwa muda mrefu kwa ajili ya matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment