Friday 4 December 2015

UNAHISI NI NINI KINAPELEKEA VIJANA KUWA MATAPELI WA AINA HII?

MTU  mmoja ajulikaye kwa jina la James Charles (27) mkazi wa Kijiji cha Nyamori Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma, anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huku akizitumia kuwataperi wananchi.
James Charles (27)  aliyekamatwa na Jeshi la Polis Mkoani Kigoma akifanya utapeli kwa kutumia sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ)



Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ferdinand Mtui, aliiambia Blog hii kuwa, mtuhumiwa alikamatwa siku ya Octoba 30 majira ya saa 8:30 mchana katika kijiji cha Kazuramimba Wilaya ya Uvinza mkoani hapa akifanya utapeli kwa kutumia sare hizo.

Kamanda Mtui alisema kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatapeli wananachi huku akiwaambia yeye ni Afisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania huku sehemu zingine akiwaambia nafanya kazi za maafisa uhamiaji.



“Kabla ya kukamatwa alikuwa ameshachukua pesa za wananchi Tsh. 900,000/= na wakati akiendelea na utapeli huo ndipo akajikuta anaingia mikononi mwa Polisi na kukamatwa” alisema Kamanda Mtui

Aidha Kamanda Mtui alibainisha kuwa, hii si mara ya kwanza kwa mtuhumiwa huyo kukamatwa na Sare hizo kwani awali alishawahi kukamatwa akifanya utapeli huo na alifungwa kifungo cha nje.

“Wakati akitumikia kifungo cha nje bado aliendelea kutapeli watu kwa kutumia sare hizo hivyo tunaweza kumuita ni mtuhumiwa sugu kutokana na kukaidi agizo la mahakama” aliongeza Kamanda Mtui


Hata hivyo Kamanda Mtui aliwataka wananchi wote ambao walitapeliwa na Mtuhumiwa huyo kutoa taarifa katika vituo vyovyote vya  Polisi vilivyo karibu yao ili kujua idadi ya watu ambao walishatapeliwa ili ijulikane watu wangapi wanatakiwa kurudishiwa pesa walizotapeliwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!