Tuesday 8 December 2015

SERIKALI YAONGEZA SH 132 BILIONI KWA BODI YA MIKOPO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya

Dar es Salaam. Zaidi ya wanafunzi 52,000 wa mwaka wa kwanza watanufaika na mkopo wa elimu ya juu baada ya Serikali kuongeza fedha kiasi cha Sh132 bilioni, kwa ajili ya kugharamia masomo yao kwa mwaka wa masomo wa 2015/16.


Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Hamis Chagonja alisema bajeti ya Sh341 bilioni ilikuwa imetengwa kwa ajili ya wanafunzi 14,226 wa mwaka wa kwanza.
Hata hivyo, alisema Serikali imeongeza fedha hizo hadi kufikia Sh473 bilioni ambazo zinatosha kuwalipa wanafunzi 52,000. Alisema ongezeko hilo litawawezesha wanafunzi wengine 37,774 ambao hawakuwamo kwenye bajeti kudhaminiwa na bodi yake kwa mwaka huu wa masomo.
“Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni 71,125 hatuna shida sana, wao wataweza kupata fedha hizo. Changamoto ilikuwa kwa hawa wa mwaka wa kwanza, lakini sasa tumepata fedha za kuwalipa,” alisema
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!