Thursday, 10 December 2015

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA RWANDA AKAMATWA

Image copyrightGetty
Image captionNtaganzwa ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakitafutwa sana
Marekani inasema kuwa mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika pakubwa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, amekamatwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Ladislas Ntaganzwa, ambaye ni meya wa zamani, anatuhumiwa kwa kuwaua maelfu ya watu na kupanga ubakaji wa jumla mwaka huo wa 1994.
Ni mmoja kati ya washukiwa tisa wakuu wanaosakwa na Umoja wa Mataifa.
Wengine wanane bado hawajulikani waliko.
Marekani ilikuwa imeahidi zawadi ya dola 5 milioni kwa atakayesaidia kukamatwa kwake.
NtaganzwaImage copyrightOther
Image captionNtaganzwa ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakitafutwa sana
Idara ya ulinzi nchini Rwanda imekuwa ikimtuhumu kwa kuwa mchochezi mkuu na mpangaji wa mauaji ya kimbari katika wilaya ya Butare, kusini mwa Rwanda.
BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!