Thursday 3 December 2015

MPYA: WAZIRI MKUU MAJALIWA NDANI YA BANDARI TENA,MAKONTENA ZAIDI YA 2000 YAMEPITA BILA KODI


Waziri Mkuu afanya ziara ya kushtukiza tena bandarini na Shirika la Reli (TRL) Dar, akuta makontena 2431 yamepita bila kodi, atoa saa 3 majina yote yapatikane.

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na shirika la reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.

Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.

Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.

VIA-JMF

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!