Pages

Thursday, 31 December 2015

MATUKIO MWAKA 2015


Mwenye Kipindi cha In my Shoes na aliyekua mpenzi wake Diamond Platinum, Miss Wema Sepetu agombea Ubunge wa viti maalum CCM.
Mwigizaji huyu maarufu wa filamu pia ana support ya kutosha toka wa mama yake mzazi katika kufanikisha nia yake ya Ubunge.





WATANZANIA ni miongoni mwa jamii ya kimataifa ambayo imetingwa na mambo mengi ya kisiasa kwa mwaka 2015.
 Mwaka 2015 Tanzania ilitingwa na mambo mengi ya kisiasa ikiwa ni pamoja kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kuvunjwa kwa Bunge la Kumi na uchaguzi mkuu. Mwaka huu umeweka historia ya kumalizika kwa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete na kuanza kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.





Umoja huo ulioundwa na NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na chama cha National League for Democracy (NLD) uliamua kumsimamisha Edward Lowassa kugombea urais ili kutimiza lengo lao la kushirikiana katika masuala ya kisiasa kwa lengo la kuking’oa madarakani chama tawala. wwKatika ulingo wa siasa pia kumekuwa na historia baada makada wa CCM waliowahi kushika nafasi ya waziri mkuu , Frederick Sumaye na Edward Lowassa kujiondoa kwenye chama hicho na kujiunga na kambi ya upinzani wakifuatiwa na kada mkongwe Kingunge Ngombale-Mwiru.

Daftari la kudumu la Wapiga Kura Mwaka 2015 Tanzania imeweka historia ya kuimarisha mfumo mpya wa uandikishaji wa wananchi katika daftari la kupiga kura kwa mfumo wa Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) toka kwenye Teknolojia ya awali iliyozoeleka ya “Optical Mark Recognition” (OMR). Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar zimeboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kufikisha watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea tayari wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikadiria kuandikisha wapiga kura wapatao 24,253,541 kulingana Taarifa ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) lakini mpaka zoezi linakamilika, walioandikishwa kwa nchi nzima walikuwa wapiga kura wapatao 23,782,558 sawa na asilimia 98.06. Taarifa zote hizo za mpiga kura zitahifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) na BVR itaweza kwa asilimia kubwa kusaidia, kuondoa wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya mara moja, kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi na kuhamisha wapiga kura waliohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Kama ilivyo kwa mabunge yaliyopita, Bunge la Kumi lilikuwa na jumla ya mikutano 20 kwa mgawanyo wa mikutano minne kila mwaka. Taarifa ziliwasilishwa na kujadiliwa na Bunge na hatimaye Bunge kuazimia kuitaka Serikali kuchukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya mawaziri na watendaji wa serikali. Mijadala hiyo ni pamoja na Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na Miamala iliyofanyika katika Akaunti ya ESCROW ya Tegeta, umiliki wa IPTL na taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu zoezi la Operesheni Tokomeza.
Bunge la Kumi liliondokewa na wabunge 10 waliofariki dunia kwa nyakati tofauti akiwamo Mussa Khamis Silima wa Baraza la Wawakilishi na Regia Estelatus Mtema (Viti Maalum-CHADEMA) waliofariki kwa ajali. Wabunge wengine nane walifariki kwa ugonjwa ambao ni Jeremiah Solomon Sumari (Arumeru Mashariki-CCM). Wengine waliofariki kwa ugonjwa ni Salim Hemed Khamis (Chambani-CUF), William Agustao Mgimwa (Kalenga-CCM), Said Bwanamdogo (Chalinze-CCM), Capt John Damiano Komba (Mbinga Magharibi-CCM), Eugen Elishilinga Mwaiposa (Ukonga-CCM).
Donald Kelvin Max- (Geita-CCM), Mariam Mfaki Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma (CCM). Bunge hilo lilishuhudia kujiuzulu kwa wabunge wawili ambao ni Rostam Aziz aliyekuwa anawakilisha Jimbo la Igunga (CCM) ambaye aliyejiuzulu ubunge kwa hiari. Pia Kabwe Zitto aliyekuwa anawakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) aliondoka bungeni baada ya kupoteza sifa ya kuwa Mbunge kutokana na kupoteza uanachama wa chama chake cha Siasa.
Uchaguzi Mkuu na historia ya kipekee Mwaka huu Watanzania wamejitokeza na kupiga kura katika hali ya amani na utulivu na kuchagua madiwani, wabunge na rais atakayeunda serikali ya awamu ya tano. Idadi kubwa ya watu walijitokeza na kujiandikisha kupiga kura. Kwa mujibu wa takwimu Tume ya Uchaguzi, idadi ya wanawake waliojiandikisha kupiga kura ni 11,950,200 na idadi ya wanaume 10,800,589.

Wagombea wanane wa nafasi ya urais wamepigiwa kura ili kumpata rais atakayeongoza serikali ya awamu ya tano kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020. Walioshiriki kugombea urais ni Dk John Magufuli (CCM), Edward Lowassa (CHADEMA) ambaye aliwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) , MacMillan Lyimo (TLP) na Chief Lutalosa Yembe na Said Miraj Abdallah (ADC). Pia Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP), Hashim Rungwe (CHAUMMA), Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) na Janken Kasambala (NRA).

Uchaguzi wa mwaka huu umeweka historia ya kipekee kutokana na mambo mbalimbali yaliyojitokeza katika kipindi cha kampeni na baada ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi mkuu, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ilitangaza kufuta matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 baada ya kubainika kujitokeza kwa kasoro nyingi, zilizosababisha kukiukwa kwa sheria za uchaguzi na haki kushindwa kutendeka.
Mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiwasalimu wananchi mjini Rais mstaafu Jakaya Kikwete Kigoma alipokwenda kuwaomba kura.
Ni mara ya kwanza kwa CCM kumteua mwanamke kushika nafasi ya juu tangu chama hicho kilipoanzishwa mwaka 1977. Pia ACT-Wazalendo imeweka historia ya kipekee kwa kuwa chama cha kwanza kumteua mwanamke, Anna Mghwira, kugombea nafasi ya urais jambo linalohamasisha jamii kujenga usawa wa kijinsia katika uongozi wa kisiasa. Jambo lingine lililowezesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kuwa wa kipekee ni uamuzi wa vyama vinne vya kambi ya upinzani kutumia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kusimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya urais kupitia Chadema.
Pia kuimarika kwa ushirikiano kati ya Tume ya Uchaguzi na vyombo vya habari kumeweka historia mpya ambapo vituo vya redio na televisheni vimeruhusiwa kurusha moja kwa moja matukio ya uchaguzi kwa saa 24 pamoja na matokeo ya uchaguzi. Mwaka huu umeweka historia ya kumalizika kwa Serikali ya Awamu ya Nne, ambapo Rais Kikwete amewaaga Watanzania na kuwahimiza kutoa ushirikiano kwa Rais John Magufuli kwa kuwa ana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli.



Rais Kikwete alisema baada ya kustaafu. Baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Magufuli aliandika historia ya kuwa Rais wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano Novemba 5, mwaka huu.
Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli amekuwa akifanya maamuzi yanayoibua gumzo miongoni mwa Watanzania na dunia kwa ujumla ikiwemo kufuta sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kuagiza fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya sherehe hizo kiasi cha Sh bilioni nne zitumike katika shughuli nyingine za maendeleo hususan upanuzi wa barabara.
Pia Rais Magufuli ameweka historia ya kukaa muda mrefu kabla ya kuchagua baraza lake la mawaziri, kufuta safari za nje ya nchi kwa viongozi na watendaji wa serikali na kuzuru ofisi mbalimbali za serikali kwa ghafla na kuwawajibisha viongozi wanaodaiwa kuzembea. Mwaka huu wa 2015 umekuza demokrasia na kuwafanya Watanzania kuwa na mwamko wa kufuatilia duru za siasa.




YALIYOJIRI MWAKA 2015: Ajali zatesa na kurudisha nyuma taifa





Kwa mwaka huu, tumeshuhudia ajali nyingi za barabarani zikichukua uhai wa watu wengi wasio na hatia. Ajali hizi huhusisha vyombo vya moto, zikiwemo pikipiki na magari. Pamoja na vifo hivyo, lakini Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi kinasema ajali za barabara zimepungua hadi 7,570 kwa kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka huu, ikilinganishwa na ajali 13,466 zilizotokea kwa kipindi kama hicho mwaka jana.
Kamanda wa Kikosi hicho, Mohamed Mpinga anasema katika ajali hizo, vifo vilipungua kutoka 3,437 mwaka jana hadi vifo 3,195 mwaka huu huku majeruhi wakipungua kutoka 13,495 mwaka jana hadi 8,566 mwaka huu. Anasema kwa mwezi Januari mwaka huu, ajali zilikuwa 823 zilizosababisha vifo 273 na majeruhi 876 ; huku mwaka jana ajali zilikuwa 1,864 zilizosababisha vifo 320 ambapo majeruhi walikuwa ni 1,529.
Kwa mwezi Februari mwaka huu, zilitokea ajali 641 na kusababisha vifo 236 huku majeruhi wakiwa 726, ambapo kwa mwaka jana Februari ajali zilikuwa 1,610 zilizosababisha vifo 220 na majeruhi 1,338. Mpinga anasema kwa mwezi Machi mwaka huu, ajali zilipungua hadi 652 na kusababisha vifo vya watu 357 na majeruhi 761 ; huku Machi mwaka jana ajali zilikuwa 1,419 na kusababisha vifo 314 na majeruhi 1,277.
Anasema kwa Aprili mwaka jana, ajali zilikuwa 1,211 zilizosababisha vifo 278 na majeruhi 1,166, ambapo kwa mwezi Aprili mwaka huu zimepungua hadi 602 na kusababisha ajali 327 na majeruhi 815. Mpinga anasema kwa Mwezi Mei mwaka jana, ajali zilikuwa 1,144 zilizosababisha vifo 291 na majeruhi 1,024, ambapo kwa Mei mwaka huu zilitokea ajali 611 na kusababisha vifo 257 na majeruhi 627.
Katika mwezi Juni mwaka jana, zilitokea ajali 1,157 na kusababisha vifo 320 na majeruhi 1,189, ambapo kwa mwezi Juni mwaka huu, zilitokea ajali 750 na kusababisha vifo 297 na majeruhi 1,021. Aidha, kwa upande wa mwezi Julai mwaka jana ajali zilikuwa ni 1,035, zilizosababisha vifo 368 na majeruhi 1,261, ambapo Julai mwaka huu ajali zilikuwa 776 na kusababisha vifo 342 na majeruhi 871.
Kamanda huyo anaeleza kwamba kwa mwezi Septemba mwaka jana, ajali zilitokea 958 zilizosababisha vifo 339 na majeruhi 1,166, ambapo mwezi kama huo mwaka huu zilitokea ajali 675 na kusababisha vifo 277 na majeruhi 806. Anasema kwa Oktoba mwaka jana, zilitokea ajali 1,020 na kusababisha vifo 322 na majeruhi 1,115. Oktoba mwaka huu zilitokea ajali 620 na kusababisha vifo 278 na majeruhi 678.
Kwa mwezi Novemba mwaka jana, zilitokea ajali 902 na kusababisha vifo 275 na majeruhi 1,065 ambapo kwa Novemba mwaka huu zimepungua na kufikia ajali 720, zilizosababisha vifo 238 na majeruhi 664. Anasema ajali hizo zimepungua kutokana na elimu ya usalama barabarani inayoendelea kutolewa kwa wananchi. Anasema kwa wastani, ajali za kila mwezi zimepungua kutoka zaidi ya 1,000 kwa mwaka jana na chini ya 1,000 kwa mwaka huu.
Anasema mara nyingi kipindi cha kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ajali nyingi hutokea na kusababisha vifo na majeruhi na kutoa elimu za mara kwa mwaka na kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuyatumia magari yao vizuri na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali hizo. “Tatizo kubwa la ajali za barabarani ni mwendokasi, magari mabovu, ulevi na kupita gari la mbele bila tahadhari, hivyo madereva wafuate sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali hizi, “ anaeleza.

Kutokana na kukithiri kwa ajali za barabarani, Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) wanatoa wito kwa serikali na wadau wa usalama barabarani, kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani, ambazo zimekuwa zikikatisha uhai wa Watanzania wengi wasio na hatia. Pia wanatoa wito kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kufanya ukarabati wa mara kwa mara wa barabara ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
Kwa upande wake, Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kinasema kwa sasa barabara imekuwa si salama tena, imekuwa ni sehemu ya mauaji, kutokana na kuteketeza maisha ya wananchi wengi kwa wakati mmoja.

Sehemu ya mbele ya basi la Moro Best likiwa limeharibika baada ya ajali hiyo.
Sehemu ya mbele ya basi la Moro Best likiwa limeharibika baada ya ajali hiyo na mabomba kutoka kwenye lori yakionekana.
 print
Baadhi ya majeruhi wa basi la Moro Best lililopata ajali baada ya kugongana na lori katika eneo la Pandambili wakati likitokea Mpwapwa kwenda Dar es Salaam.
Baadhi ya majeruhi wa basi la Moro Best lililopata ajali baada ya kugongana na lori katika eneo la Pandambili wakati likitokea Mpwapwa kwenda Dar es Salaam.
Inaelezwa kuwa la Moro Best lilikuwa likitokea Dodoma kuelekea Morogoro na kuwa katika ajali hiyo watu zaidi ya 12 walikufa papo hapo na wengine watano wamefia njiani wakati wakipelekwa hospitalini kutibiwa.

AJALI zimekuwa ni janga linalorudisha nyuma maendeleo ya Watanzania wengi kwa kusababisha vifo, majeruhi na kuwaacha watu wengine wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo.


GOSSIP ZA MASTAA NA MENGINEYO:
“Kubuni mbinu za kuwateka mashabiki, nayo ni moja ya mbinu ninazofanya kila siku,” alisema Diamond.
Hatimaye Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz, ametoa siri ya mafanikio yake kimuziki.
“Kubuni mbinu za kuwateka mashabiki, nayo ni moja ya mbinu ninazofanya kila siku,” alisema Diamond.
Amesema kinachomfanya azidi kupaa, ni kujituma na kuwa mbunifu kila siku.
“Nafanya kazi zangu kwa bidii, nazingatia ubunifu na kufanya mazoezi mara kwa mara.
“Kubuni mbinu za kuwateka mashabiki, nayo ni moja ya mbinu ninazofanya kila siku,” alisema Diamond.
DIAMOND & ZARI  ndio wapenzi waliotingisha na waliovuma zaidi  2015.




Wema Sepetu blesses Platnumz and Zari

Diamond Platnumz' ex lover, Wema Sepetu, has said she has no problem with Diamond dating ... I know I have learnt and for sure can't make the same mistakes I made earlier. God I pray for 2015 to be my year and I'm gonna make it my walk to remember."




No comments:

Post a Comment