Matembezi ya maadhimisho ya siku ya watoto wa vichwa vikubwa na Mgongo wazi yaliyoanzia Kariakoo na kuishia Taasisi ya Mifupa Muhimbili(Muhimbili) yamefanyika leo mapema jijini Dar.
Lengo la matembezi hayo ni kuwapa moyo na ushirikiano wazazi wenye watoto waliozaliwa na tatizo hilo la vichwa kujaa maji, tatizo linalosababishwa na mama mjamzito kuwa na upungufu wa madini ya folic acid mwilini. madini ambayo hupatikana katika vyakula kama mboga za majani na matunda .
Aine Abel Ngapemba akiwa na bango wakati wa Matembezi ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi yalianzia Kariakoo na kuishia Hospitali ya Taifa Muhimbili
Mdau Anna Peter Apema akiongea na kupata maelezo toka kwa mmoja wa wazazi wenye watoto waliozaliwa na tatizo la kichwa kujaa maji.
Asilimia zaidi ya tisini wamekimbiwa na waume zao,na hali
hiyo inawafanya wamama hao kulia sana wakiwa wodini,kiukweli wanahitaji upendo sana kutoka kwetu.
No comments:
Post a Comment