Saturday 26 December 2015

KRISMASI YA MBU , NZI NA FUNZA KWA WALE WA MABONDENI




Wakati dunia ikisherehekea sikukuu ya Krismasi kwa furaha jana, familia zaidi ya 500 za wakazi waliokuwa wakiishi bonde la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam, walikuwa na machungu ya aina yake kutokana na dhiki kubwa waliyonayo tangu kubomolewa nyumba zao wiki iliyopita.
 
Nipashe imefanikiwa kuzungumza na waaathirika wa bomoa bomoa hiyo ambao wameeleza maisha mapya baada ya zoezi hilo ambapo wengi wao wamekuwa wakilala juu ya vifusi vilivyotokana na kubomolewa kwa nyumba zao.
 
Katika maeneo mengi ambapo mwandishi alitembelea, wakazi hao walionekana wakiwa wameegesha mabati na mbao kama yalivyo mabanda ya mamalishe ambayo huyatumia kwa malazi jua linapozama. Zoezi hilo lililoanza Desemba 17 na kusitishwa Jumanne, limeacha simanzi ya aina yake kwa familia za wakazi hao ambao wengine wamedumu maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 30.
 
Zaituni Bushiri ambaye ni mpangaji katika moja ya nyumba mtaani hapo alisema mbu, nzi na wadudu wakiwamo funza ni sehemu ya maisha yao kwani maji machafu yanayotoka vyoo vya nyumba zilizobomolewa yamekuwa yakitiririka kuelekea kwenye maeneo yao muda wote. Alisema kutokana na mazingira yao kuwa machafu wana hofu ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu muda wowote kwani hata sehemu waliyokuwa wakiitumia kama jalala hivi sasa kuna wananchi wameezeka vibanda na kulala hapo. Kwa mujibu wa mjumbe wa shina No. 10, Kikozize Abdallah, wakazi ambao wamerejea katika eneo hilo  ambao ni zaidi ya 500 hawana vyoo vya kujisitiri.
 
Abdallah alisema, mchana wananchi hao wamekuwa wakijisaidia kwa kuomba omba kwa majirani ambao nyumba zao zilisalia kwenye zoezi la bomoa bomoa.
“Usiku ndipo shida inapokuja maana huwezi kupita kwenye vifusi vyote kutafuta choo kwenye nyumba za watu, hivyo tunajisaidia humu humu kwenye maeneo tunayoishi,” alisema.
 
 Zuhura Hashim alisema wanawake ndio wenye changamoto kubwa kwenye maeneo hayo kwa sababu ya maumbile yao na hawawezi kujisaidia na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta vyoo. Maria Mlanga, mkazi wa mtaa huo, aliyekuwa akiishi nyumba ya urithi wa mkwe wake, alisema kwa sasa wanaishi maisha ya kuokoteza okoteza baada ya kupoteza vitu vyao vyote wakati nyumba yao ya vyumba vitatu ilipobomolewa na tinga tinga la Jiji.
WATOTO WOTE
 
Alisema wamelazimika kurudi katika eneo hilo baada ya kukosa mahali pa kwenda kwasababu walikuwa wakiishi familia nzima na hakuna mtu aliyejitokeza kuwasaidia hifadhi. “Siyo kwamba hatuna ndugu, ila tunawezaje kwenda kuishi nao na watoto wote hawa,” alisema Mlanga mwenye watoto watatu. “Kwa hiyo naona ni bora nitafute hifadhi ya watoto hapa hapa ilipokuwa nyumba yetu wakati nikiendelea kubangaiza maisha ili wapate angalau milo miwili kwa siku. “Tumeshtukizwa, heri wangetuambia mapema tukawahi kuondoa hata vitu au kuhama wenyewe kwa hiyari, ilikuwa ghafla hatukutarajia. “Watoto walikuwa shule na wengine tulikuwa kwenye shughuli zetu tulirudi na kukuta kibanda chetu kimegeuzwa kifusi, kwa kweli nilipata mshtuko. “Nilikuwa na vitu vyangu ndani ya kibanda changu, nilikuwa nimejijenga kimaisha, kwa sasa sina kitu zaidi ya godoro na nguo nilizofanikiwa kuziokoa, nitaenda kuanzaje maisha kwingine wakati sina kitu? 
 
“Nitabaki hapa hapa hadi serikali itakapotupatia eneo lingine.”
Alisema kubomolewa kwa nyumba yake kumemsababishia msongo wa mawazo na sasa anakabiliwa na shinikizo la damu linalosababisha apoteze fahamu mara kwa mara.
 
NYAKATI ZA USIKU
Said Mohamed, ambaye naye ni mkazi wa eneo hilo aliyekuwa na nyumba ya wapangaji kwa zaidi ya miaka 30, alisema wananchi wengi waliobomolewa wamekosa pa kwenda na wameendelea kuishi juu ya mabaki ya nyumba zao na wengi wao wamekuwa
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!