Tuesday, 8 December 2015

KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS YAKABIDHI VIFAA VYA USAFI VYA MILIONI 5.5 MANISPAA YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO‏




 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (wa tatau kulia), akimkabidhi vifaa mbalimbali vya usafi wa mazingira vyenye thamani ya sh.milioni 5.5, Katibu Tawala (DAS), wa Wilaya ya Temeke, Laurence Mlangwa Dar es Salaam leo mchana, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema kwa ajili ya kusaidia kufanyia usafi leo hii ikiwa ni kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kutumia Sikukuu ya Uhuru kufanya usafi nchini kote. Kulia ni Ofisa Usalama na Mazingira wa Puma, Jonathan Mmari na wengine ni maofisa kutoka Manispaa ya Temeke

 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo.
 Ofisa Usalama na Mangira wa Puma, Amani Mmari (kulia) akizungumza katika mkutano huo wa makabidhiano wa vifaa hivyo. Wa pili kulia ni Meneja Rasimali Watu (HR) wa Puma, Loveness Hoyange.
 Vifaa hivyo vikikaguliwa.
 Mkurugenzi wa Puma akitoa maelekezo wakati wakikabidhi vifaa hivyo.
 Vifaa hivyo vikipangwa katika toroli.
 Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo.
 Baadhi ya vifaa hivyo.
 Matoroli yaliyokabidhiwa na Puma kwa Manispaa ya Temeke.
Matoroli yakipakiwa katika gari la Manispaa ya Temeke baada ya kukabidhiwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma imetoa vifaa vya usafi wa mazingira vyenye thamani ya sh.milioni 5.5 kwa manispaa ya Temeke ili kutekeleza agizo la Rais John Magufuli alilotaka kila mmoja wetu kushiriki kufanya usafi katika kilele cha Sikukuu ya Uhuru ambayo inafanyika nchini kote leo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Laurence Mlangwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti alisema aliguswa mno na agizo la Rais na kuona ni vema Puma nao wakamuunga mkono rais.

"Baada ya kusikia katika vyombo vya habari kuwa rais ameagiza katika sikukuu ya uhuru mwaka huu badala ya kufanya sherehe  hufanyike usafi niliguswa na kuamua kumuunga mkono" alisema Corsaletti.

Alisema wameamua kutoa vifaa hivyo kwa manispaa ya Temeke ili kusaidia kazi ya usafi katika maeneo mbalimbali ambao utafanyika leo nchini kote.

Alitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni matoroli 10, mipira ya kuvaa mikononi wakati wa kufanya usafi, viatu vya mvua, vizibao na vinginevyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 5.5

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Manispaa hiyo Laurence Mlangwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, aliishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa vifaa hivyo ambapo alisema vifika wakati muafaka ambapo leo vitatumika kufanyia usafi kama Rais Magufuli alivyo agiza.

Alisema shughuli za usafi huo zitaanzia viwanja vya Mbagala Zakhem na kutawanyika kuelekea maeneo mengione mbalimbali.




No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!