Tetenasi ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria wanaoitwa ( Clostridium tetani). Wadudu hawa wanapatikana katika mazingira yanayotuzunguka mfano; ardhi,misumaru au vitu vyenye ncha, vinyesi vya baadhi ya wanyama nk. Bacteria wa tetenasi wanaweza kuishi katika mazingira kwa miaka mingi .
Pia wanapenda vidonda, ndio maana wanaingia mwilini kupitia vidonda au mikwaruzo. Dalili za Tetenasi zinatokea siku 4-14 baada ya kupata jeraha. Tetenasi imegawanyika sehemu mbili: 1. Tetenasi inayotokea kwa watu wazima (adult) 2. Tetenasi ya watoto (neonates)
NANI YUPO HATARINI KUPATA TETENASI? KWA WATU WAZIMA(ADULTS) 1.
Ikiwa umeumia na kupata jeraha au kidonda sehemu ya mwili wako uko katika hatari ya kupata ugonjwa huu hatari wa tetenasi. 2. Ikiwa umetobolewa na msumari una zaidi ya 32% kupata tetenasi 3. Ikiwa umeungua, au watu wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya, au watu wanaojiwekea tattoo, watu wenye magonjwa ya meno, wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu 4. Kisukari ni moja ya hali inayoweza kukusababishia tetenasi 5. Pia upasuaji (surgery) isiyo salama, mfano matumizi ya vyombo visivyo salama(unsterilized)
KWA WATOTO 1. Kama mama mjamzito hatapata chanjo ya tetenasi , au kujifungulia nyumbani, yupo kwenye hatari ya kumsababishia mtoto mchanga kupata tetenasi.
DALILI ZA TETENASI 1. Kukakamaa kwa misuli, mdomo kushindwa kufunguka(lock-jaw) 2. Kutokwa na jasho jingi, homa kali 3. Kushindwa kumeza kwasababu ya kukakamaa kwa misuli. 4. Kutokwa na udenda(drooling) 5. Kupata matatizo ya kupumua.
KINGA; - Tafadhali nenda hospitalini au kituo cha afya mara baada ya kupata jeraha lolote ili kupata chanjo ya tetenasi - Kwa wafanyakazi wa afya, ni muhimu kupata chanjo ya tetenasi kwasababu ya mazingira hatarishi ya kazi.
Kwa mama mjamzito tafadhali hakikisha unapata chanjo zote za tetenasi ili kujikinga na pia kumkinga mtoto. Pia unapoona dalili za uchungu hakikisha unawahi ukajifungulie kituo cha afya mapema. -
Epuka majeraha yasiyokua ya lazima, vaa viatu, weka vitu vyenye ncha kali mbali na watoto. -
Mpeleke mtoto atahiriwe hospitalini na sio kwa mtaani, kwasababu ya hatari kubwa iliyopo ya kupata tetenasi.
Chanjo ya Tetenus ni chanjo inayotolewa kwa watu wote ili kujilinda na madhara ya maambukizi ya bakteria anayeitwa clostridium teteni, bakteria huyu anapoingia mwilini hutoa sumu inayosababisha kuharibu kwa usafilishaji wa taarifa za mishipa ya fahamu ya misuli. Matokeo yake ni mtu huanza kupata dalili mbalimbali kama zilivyotajwa hapo chini.
Wakati gani wa kupata chanjo ya tetenus
Serikali imeweka utaratibu kwa wanawake kupata chanjo bure kabisa katika vituo vya afya hasa ngazi ya wilaya(kwa nchi ya Tanzania) kwa ujumla mwanamke anatakiwa kupata chanjo tano kipindi chake cha uzazi ambazo hutolewa kama ilivyoandikwa katika jedwali hapo chini
Vihatarishi vya kupata tetenus
Bakteria wanaosababisha tetenus lazima wawe na njia ya kuingia mwilini ndipo wasababishe tetenus ambapo hata hivyo vihatarishi vinavyomuweka hatarini mtu kupata tetenus ni kama vile
- Kutokupata chanjo, kutopokea chanjo inayofuata dhidi ya tetenus ama kuacha kuendeleza kupokea chanjo kama inavyotakiwa
- Jeraha linalozama ndani ya mwili linalosababisha bakteria wa tetenus kuingia ndani ya mwili kupitia mlango huo
- Kuwepo kwa bakteria wanaosababisha tetenus
- Jeraha lolote
- Kutobolewa na kitu kama msumali,n.k
Tetenus pia hutokea kwa watu wenye majeraha kama yafuatayo
- Majeraa ya kujikata- kujigonga na nyundo, kujitoboa na pini ama kuchora tatuu ama kujidunga madawa ya kulevya
- Jeraha kutokana na kupigwa risasi
- Jeraha ya kuvunjika mifupa
- Jeraha la kusagika kwa maungio yoyote ya mwili ama misuli, ngozi
- Majeraha kutokana na kuungua moto
- Majeraha ya upasuaji
- Majeraha kutokana na kuchoma sindano
- Maambukizi ya masikio
- Kungatwa na wanyama
- Vidonda visivyo visafi katika miguu
- Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto ambacho bado hakijakauka kutoka kwa mama ambaye hajapata chanjo kama inavyotakiwa
No comments:
Post a Comment