Wednesday 23 December 2015

AUWAWA KWA KUCHINJWA AKIWA NYUMBANI KWAKE CHUMBANI AMELALA



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Kazimili (49) Mkazi wa Kitongoji cha Misenga Tarafa ya Mwese ameuwawa kikatili kwa kukatwa katwa na  shoka na mapanga katika  sehemu mbalimbali za mwili wake wakati akiwa amelala chumbani kwake na mke wake.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa tukio la mauwaji hayo ya kikatili lilitokea hapo  juzi majira ya saa saba usiku nyumbani kwa marehemu huyo .

Alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala kwenye nyumba yake ndani ya  chumba chake akiwa na mke wake waliyekuwa wakiishi nae pamoja na watoto wake .
Kidavashari alieleza wakati marehemu akiwa amelala ndani  watu wasiofahamika walifika nyumbani kwake na kuvunja mlango wa mbele wa nyumba yake hiyo huku wakiwa na silaha  aina ya shoka na mapanga.

 Baada ya kuwa wamevunja mlango wa mbele watu hao waliingia ndani hadi mahali alipokuwa amelala marehemu na mkewe  na kisha walimtowa  sebuleni marehemu huku wakiwa wamemlazimisha mkewe asitoke nje wala asipige kelele.

Kidavashari alieleza baada ya kuwa wamemtowa sebuleni walianza kumshambulia kwa kumkatakata kwa  silaha za  panga na shoka katika seheme  mbalimbali  za mwili wake   za kichwani shingoni na  kwenye mikono yake  huku marehemu huyo akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada  kwa majirani zake.

 Alisema pamoja na marehemu kupiga mayowe   wauwaji hao hawaku jali na waliendelea kumkatakata marehemu hadi walipoona amefariki dunia  ndipo walipotokomea  kusiko julikana.

Majirani walifika kwenye eneo hilo na  walikuta mwili wa marehemu ukiwa umegalagala chini huku ukiwa umekatwa katwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Kidavashari alisema mpaka chanzo cha  kifo hicho cha mauwaji ya kikatili hakijafahamika  na jeshi la pollsi wa kushirikiana na wananchi wa Kitongoji hicho wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliohusika  na mauwaji hayo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!