Wednesday, 16 December 2015

ATHARI YA KULA NYAMA NYEKUNDU 'RED MEAT':






Tafiti za hivi karibuni imebaini kwamba sehemu kubwa ya maisha yetu inaathiriwa na ulaji na unywaji usio sahihi.



,Ulaji na unywaji huu ndiyo unaosababisha magonjwa ya aina mbalimbali kama saratani ya tumbo,utumbo,njia ya haja kubwa na hata tezi dume'prostate gland'.Wengi wamekuwa wakitumia nyama nyekundu bila kufahamu madhara yake(nyama nyekundu ni ya n'gombe,kondoo,mbuzi,nguruwe nk).

Kilishe nyama nyekundu ni nyeti kwa mwili wa binadamu lakini inapoliwa kupita kiasi ni tatizo,kwa kawaida binadamu anatakiwa kula nusu kilo tu ya nyama nyekundu kwa wiki(siku saba)lakini walio wengi hula nusu kilo au zaidi kwa siku matokeo yake kuwepo hatari kubwa ya kupata saratani ya utumbo mkubwa,athari ya viungo'gout' na utafiti unaonyesha kwamba ulaji wa zaidi ya nusu kilo huzidisha hatari kwa asilimia 15% na pia watu wanaokula nyama nyekundu zaidi ya mara 8 kwa wiki wana asilimia 50% kupata upofu ukilinganisha na wale wanaokula nyama hiyo chini ya mara tano kwa wiki.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!