Rais wa Syria Bashar al-Assad amelaani hatua ya Uingereza kufanya mashambulizi nchini mwake akisema sio halali.
Katika mahojiano na gazeti la Sunday Times, rais Assad anasema kuwa mashambulizi ya ndege za kijeshi za Uingereza dhidi ya kundi la wanamgambo wa Daesh ama Islamic State ni kinyume na maadili ya kimataifa na inakiuka uhuru wa taifa lake.
Bwana Assad anasema mashambulizi hayo yanakoleza na kueneza saratani ya ugaidi.
Rais huyo alilinganisha mashambulizi yanayoendeshwa na Urusi na hayo yanayoendeshwa muungano wa mataifa ya magharibi yakiwemo Ufaransa na Marekani, akidai kuwa mashambulizi ya Urusi yaliyofanywa kwa ushirikiano na jeshi la Syria ndiyo yaliyochangia pakubwa kudidimizwa kwa kundi hilo la Islamic State.
Assad amesema kuwa mashambulizi ya Urusi yanasaidia kuilinda bara Ulaya.
Uingereza inasisitiza kuwa inataka kiongozi huyo wa Syria ang'atuke madarakani kinyume na mashambulizi ya Urusi ambayo yameisaidia majeshi ya Syria kukomboa maeneo yaliyokaliwa na waasi.
Majeshi ya Uingereza yalianza kuishambulia Syria siku ya Alhamisi baada ya bunge la taifa hilo kuidhinisha mswada wa kupambana na Islamic state ama Daesh
No comments:
Post a Comment