Abiria 12 wamefariki leo huku wengine 28 wamejeruhiwa mara baada ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori maeneo ya Igeme, Kilolo leo mchana.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, basi la New Force lilikuwa linatokea jijini Dar es Salaam kuelekea Tunduma, mkoani Mbeya, na baada ya kugongana na gari hilo la mizigo, yalipinduka.
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limethibisha kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi wamewahishwa hospitali ya wilaya ya Kilolo huku wengine waliokuwa taabani wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Iringa.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Iringa, madereva wa basi na lori ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo na uchunguzi unaendelea.
Picha kwa hisani ya Michuzi blog
Picha kwa hisani ya Michuzi blog
No comments:
Post a Comment