Ukitamuka maneno haya, haki sawa kwa wote, ni maneno ya busara sana na hekima, lakini kama yasipofuatwa kama yalivyo basi itakuwa ni unyanyasaji, udikiteta, uonevu na pia ni ukiukaji wa haki za binadamu ibara ya 74 kifungu kidogo cha 3.
Tangu rais magufuli aipishwe na kuapa kufuata sheria na kanuni za nchi, na kuanza ziara za hapa kwa papo watumishi wengi wa serikali wameona hali si njema kwa vile hawakuwa wakifuata sheria na kanuni za nchi katika utendaji kazi zao, haya nayasema kwa uchungu mkubwa huku nikilia kwa sauti kubwa bila kupata leso ya kufutia machozi,
Watumishi wa wizara ya ardhi wamepeleka tinga tinga (siyo rais Magufuli) katika bonde la mto msimbazi na kubomoa nyumba zote zilizojengwa katika eneo hilo bila huruma wa salie mtume!,....hawa watu wamekaidi kujenga katika eneo hili ambalo kwa sheria ya mwaka 1979 ni marufuku kujenga pembezoni mwa mito, maziwa, bahari mita 60 kutoka ukingoni,.."mkubwa wa ardhi"
Ombi langu kwa waziri wa ardhi, fukuza viongozi wote wenye dhamana hiyo kwa sababu tangu wananchi wanajenga, wanavuta umeme, maji watumishi hawa walikuwa wapi kuwapiga stop wasijenge? kama ni kuwaadhibu hawa kwa kuwavunjia nyumba basi hata watumishi wote wenye dhamana hii wapelekwe mahakama kwa kuwasababishia hasara watanzania maskini hawa, watapata wapi pesa za kujenge tena?????
HAYA NI MATOKEO YA RUSHWA KATIKA WIZARA HII ****
MDAU.
No comments:
Post a Comment