Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. Kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. Kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete wakati akiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga.
Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu, Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete. (Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment