Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana
na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa
nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na
mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa
nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na
kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia
vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara
baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu
cha Maombolezo Ubalozini hapo.
THE UNITED REPUBLIC
OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu
cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo
vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya
ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
Pamoja
na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za
pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu
na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu
Dokta
Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak
amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi
hiki kigumu cha majonzi.
Aidha
Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze
kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku
Katika
hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe
Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
Mheshimiwa
Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya
shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa
na;
Gerson
Msigwa
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November
17, 2015
No comments:
Post a Comment