Wednesday, 18 November 2015

PSPF,NHIF WASHIRIKIANA KUWAPATIA MATIBABU WANACHAMA WA MPANGO WA PSS

  Adam Mayingu na Michael Mhando wakibadilishana hati baada ya kuzisaini
 ************
Na K-Vis Media/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na NHIF.


Makubaliano hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadiz a serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilzio bora. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.


  “  Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais inatimizwa PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema Bw. Mayingu katika hotuba yake. Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha. wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla


Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, (wa pili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
  Mayingu akitoa hotuba yake
  Mhando hotuba yake
 Maafisa kutoka NHIF



 Mwanachama wa PSPF, akisoma kipeperushi, vyenye maelezo na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo
 Mmoja wa waandishi wa habari akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS
 Kaimu Murugenzi Mtendaji wa NHIF, Michael Mhando, akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro
 Mwanachama wa mpango wa Uchagiaji wa Hiari PSS, akipokea kadi ya bima ya Afya, kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omara Khalfan.
 Mwanachama wa PSPF, Constantine Edward (kushoto) akipokea kadi yake
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin, akitoa maelezo wakati wa hafla hiyo
 Meneja wa Mpango wa Uchangiajiwa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (kulia), na afisa wa PSPF, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaidika wa kwanza wa mpango wa Mfuko huo kuwapatia matibabu wanachama wake wa mpango wa PSS



Mzee Mohammed Madenge, ambaye ni Mwanachama wa PSPF, wakwanza kufaidika na mpango wa bima ya afya, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!