Monday, 16 November 2015

NDEGE ZA KIVITA ZA UFARANSA ZASHAMBULIA ISIS

Dassault Rafale


Ndege za kivita za Ufaransa zimeanza mashambulizi makali dhidi ya ngome ya Islamic State huko Raqqa huku zikiharibu kituo cha kijeshi pamoja na kambi ya mafunzo.



Taarifa kutoka jeshi la Ufaransa zinasema kuwa ndege 10 zimetumika kupiga makombora 20 kwenye malengo ya Isamic State.
Hilo ndilo shambulizi kubwa zaidi kuwahi kufanyika dhidi ya Islamic State kutoka Ufaransa na linafuatia shambulizi lililodaiwa kutekelezwa na kundi hilo mjini Paris ijumaa usiku ambapo watu 130 waliuwawa.
Mwanaume akiwa ameshika kichwa chake wakati akiweka maua akiomboleza watu waliokufa Parisn cafe, in Paris, Nov.14, 2015.Mwanaume akiwa ameshika kichwa chake wakati akiweka maua akiomboleza watu waliokufa Parisn cafe, in Paris, Nov.14, 2015.
Ndege hizo ziliondoka Jordan na jumuiya ya nchi za kiarabu Jumapili jioni zikishirikiana na vikosi vya marekani.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande alisema kuwa shambulizi la Ijumaa ni kitendo cha kivita.
Katika hatua sawa na hiyo, shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa Marekani imepeleka silaha nyingine kwa mara ya pili katika kundi la muungano wa jumuiya ya kiarabu ya Syria linalopigana na Islamic State kaskazini mwa Syria.
Chanzo:voaswahili.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!