Sunday, 15 November 2015

MSHAMBULIZI PARIS ATAJWA:OMAR MOSTEFAI

Image copyrightAFP
Image captionMshambulizi Paris atajwa:Omar Mostefai
Waendesha mashtaka wanaouchunguza matukio ya mashambulio ya kigaidi mjini Paris Ufaransa wamemtaja mmoja wa washambuliaji 7 wa kujitoa mhanga.


Omar Ismail Mostefai mwenye umri wa miaka 29 anasemekana kuwa ni raia wa ufaransa aliyekuwa anachunguzwa na polisi wa kupamabana na ugadi kabla hajatoweka.
Mtu huyo tayari alikuwa na rekodi ya uhalifu.
Omar ametambuliwa kutokana na kidole kilichopatikana katika eneo la tukio.
Image copyrightEPA
Image captionKiongozi wa mashtaka wa Ufaransa Francois Molins
Uchunguzi pia utalenga kubaini iwapo aliwahi kusafiri kwenda Syria au la .
Wachunguzi hao wanasema washambuliaji hao walijipanga katika vikundi vitatu kabla ya kutekeleza mashambulizi hayo kwa mabomu na ufyatuaji wa risasi.
Mbali na bunduki washabuliaji hao pia walikuwa na mikanda ya mabomu waliotumia kujilipua katika msururu huo wa mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu 129.
Wengi wa waliolengwa walikuwa mashabiki wa tamasha la muziki, wateja katika migahawa ,baa na hata mashabiki wa soka.
Kundi la wanamgambo wa I S wamedai kuhusika na tukio hilo.
Image copyrightAFP
Image captionRais wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari na kufunga kabisa mipaka ya taifa hilo.
Washambuliaji 7 walijilipua huku mmoja wao akipigwa risasi wakati wa operesheni ya kuokoa maisha ya watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo wa maonyesho.
Wachunguzi wanasema kuwa wanahofu kuwa washambulizi zaidi waliotoroka na sasa msako unaendelea.
Rais wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari na kufunga kabisa mipaka ya taifa hilo.
BBC:

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!