Saturday, 14 November 2015

Moja kwa Moja: Mashambulio Paris

Image captionUchunguzi mjini Paris
01.56:Watu wameondolewa katika uwanja wa ndege wa Gatwick mjini London.Maafisa wa polisi wameiambia BBC kwamba wanakabiliana na 'kitu kinachotuhumiwa'.


12.19:Viongozi wa mashtaka nchini Paris wametoa idadi ya watu waliofariki kufikia 128 huku wengine 99 wakiwa na majeraha mabaya ,kulingana na ripoti za Reuters.

Image captionRais Hollande
12.00:Wanajeshi wengine 1500 wametumwa kulinda jengo la bunge la Paris,maeneo ya kidini na vivutio vya utalii.Shule na vyuo vikuu vingi ambavyo hufunguliwa siku ya jumamosi vimefungwa ikiwa ni miongoni mwa hatua za usalama za dharura mjini humo.
11.59:Rais wa Ufaransa Francois Hollande kwa sasa anafanya mkutano wa usalama wa dharura na mawaziri pamoja na wakuu wa majeshi.
10:35 Makao makuu ya Kanisa Katoliki Vatican yametoa taarifa yakitaja mashambulio ya Paris kuwa "shambulio dhidi ya binadamu wote".
"Tunalaani (mashambulio haya) pamoja na Papa na watu wote wapenda amani," msemaji wa Vatican Federico Lombardi amesema kupitia taarifa.
10:29 Picha hii ya amani Paris yenye mchoro wa mnara wa Eiffel imekuwa ikisambazwa sana mtandaoni watu wakiwafariji watu wa Ufaransa.Mchoro huu umetoka kwa Jean Jullien.
Image copyrightOther
09:40 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameungana na viongozi wengine kushutumu uvamizi mjini Paris, na kusema mashambulio kama hayo lazima yakabiliwe kwa hatua kali. Ameahidi kutoa usaidizi na kuendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi.
09:30 Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alitisha mkutano maalum wa dharura wa baraza la mawaziri, ujulikanao kama Cobra, Downing Street kufuatia mashambulio nchini Ufaransa. Awali, alieleza kushtushwa kwake na mashambulio hayo yaliyoua watu zaidi ya 120.
09:20 Viongozi mbalimbali wameendelea kutoa risala zao
Waziri mkuu mpya wa Canada Justin Trudeau amesema wako pamoja na “binamu zetu Wafaransa wakati huu wa giza na majonzi”. Ameahidi kuisaidia serikali ya Ufaransa.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ameshtushwa sana na “habari na picha zinazotufikia kutoka Paris”. Amesema anaomboleza na waathiriwa wa “linalodhihirika kuwa shambulio la kigaidi”.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu mashambulio yaliyotekelezwa mjini Paris. Msemaji wa UN Stephane Dujarric amesema Ban ''anaamini Ufaransa ina uwezo wa kuwakamata na kuwatendea haki wahusika upesi."
09:12 Rais wa Iran Hassan Rouhani, aliyepangiwa kuzuru mji wa Roma na kisha Paris wikendi hii, ameahirisha ziara yake kutokana na mashambulio Paris.
07:50 Maafisa wa polisi wakisaidiana na wanajeshi wanashika doria maeneo mengi Paris baada ya watu 120 kuuawa katika mashambulio sita mjini humo. Hapa ni afisa wa polisi karibu na hospitali ya Saint Antoine mjini humo.
Image copyrightEAP
07:06 Raia wawili wa Sweden huenda wakawa miongoni mwa waathiriwa wa mashambulio Paris, wizara ya mashauri ya kigeni nchini humo imesema. Msemaji wa wizara hiyo Johan Tegel amesema wana habari raia mmoja wa Sweden amejeruhiwa na mwingine kuuawa.
07:00 Washambuliaji wanane wamefariki, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Saba walijilipua, na mmoja akauawa. Wanne walifariki katika ukumbi wa Bataclan, watatu kwa kujilipua na mmoja akauawa na polisi.
Watatu walifariki karibu na uwanja wa michezo wa taifa naye wa nne akauawa barabarani mashariki mwa Paris.
06:24 'Ombeeni Paris' linasema bango hili lililoinuliwa na mwanafunzi kabla ya mechi kati ya Notre Dame Fighting Irish na St Francis Red Flash uwanja wa Purcell Pavillion mjini South Bend, Marekani. Hii ni baada ya mashambulio kuua watu zaidi ya 120.
Ombeeni ParisImage copyrightReuters
Image captionWatu maeneo mengi duniani wameeleza kusikitishwa kwao na mashambulio yaliyotekelezwa Paris
06:21 Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa watu 200 wamejeruhiwa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa Paris, 80 wamejeruhiwa vibaya
Image copyrightGetty
06:12 Gazeti la Le Parisien limeandika 'Cette fois, c'est la guerre' maana yake 'Wakati huu, ni vita'.
Limechapisha takwimu za waathiriwa wa mashambulio Ufaransa, ambazo linasema limepata kutoka kwa maafisa wa polisi.
Takwimu hizo ni kama ifuatavyo:
  • Bataclan: watu 100 wamefariki, saba wamo hali mahututi, wengine wanne wanauguza majeraha
  • Rue Charonne: 19 wamefariki, 13 hali mahututi, 10 wana majeraha
  • Rue Bichat: 14 wamefariki, 10 wamo hali mahututi, 10 wengine wamejeruhiwa
  • Avenue de la Republique: Wanne wamefariki, 11 wamo hali mahututi, 10 wengine wamejeruhiwa
  • Stade de France: Wanne wamefariki, 11 wamo hali mahututi, wengine 39 wamejeruhiwa
  • Rue Beaumarchais: watatu wamo hali mahututi, wanne wengine wanauguza majeraha
05:59 Shirika la habari la Associated Press limewanukuu polisi Paris wakisema wanaamini washambuliaji wote wameuawa. Kwenye shambulio la Bataclan, ambako watu 100 wanahofiwa kufariki, washambuliaji wanne walifariki.
05:35 Magazeti duniani yalivyoripoti habari za mashambulio yaliyotokea Paris na kuua zaidi ya watu 120

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!