Friday, 13 November 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASHIRIKI MSIBA WA MJUKUU WA RAIS MAGUFULI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam,leo Nov 13, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. 
Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kulia) Makamu wake, Mh. Samia Suluhu (wa nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.

Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mjukuu wake, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mjukuu wa Mhe Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete n mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.
Baadhi ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu mjukuu wa Rais Dkt. John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Kimara,  jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, leo Nov 13, 2015.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!