Monday, 30 November 2015

"MAFISI" MBARONI DAR

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius

Wiki moja baada ya Rais John Magufuli kutangaza vita dhidi ya wauza dawa za kulevya huku akiomba wananchi kumuombea, Polisi wanamshikilia mtu mmoja kwa madai ya kujihusisha na biashara hiyo.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alithibitisha kukamatwa kwa Hussein Mafisi eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam juzi.
Rais John Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa wakati akifungua Bunge, alisema kuwa ana kazi kubwa kupambana na mafisadi, wabadhirifu, wauza unga, huku akiwataka Watanzania kumsaidia na hata kumuombea katika kazi hiyo aliyoisema ni ngumu.
Kamanda Wambura alithibitisha kukamatwa kwa Mafisi kwa madai anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Alisema kuwa polisi walipata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kuwa kuna mtu huyo anajihusisha na kuuza dawa za kulevya ndipo polisi walipofika eneo waliloelekezwa na kumtia mbaroni.
Kamanda Wambura alisema kuwa baada ya kuonyeshwa muhusika, na kwa kuwa ni maarufu, juzi walimtia mbaroni na kusema kuwa ndiye atakayesaidia polisi kuonyesha mtandao wa wauza unga. Alisema kwa sasa wanaunganisha nguvu na kikosi cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo, alipotafutwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema kuwa hawezi kuzungumza lolote kwa kuwa yuko likizo

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!