Sunday, 15 November 2015

KUFUATIA SHAMBULIZI PARIS: POLAND NA SLOVAKIA ZAKATAA KUPOKEA WAKIMBIZI

Image copyrightReuters
Image captionPoland na Slovakia zakataa kupokea wakimbizi kufuatia mauaji ya watu 139 huko Paris
Wakuu nchini Poland na Slovakia wanasema hawataki tena kutekeleza makubaliano ya Ulaya, kuwapokea maelfu ya wakimbizi waliowasili kutoka Afrika na Mashariki ya Kati katika miezi ya karibuni.


Image copyrightAFP
Image captionSlovenia tayari imeanza kujenga ua ilikuwazuia wakimbizi zaidi
Mataifa hayo yametoa ilani hiyo muda mchache baada ya rais wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker, kushauri kuwa hakuna haja ya kubadilisha sera ya umoja huo kuhusu wahamiaji, baada ya mashambulio ya Paris.
Akizungumza nchini Uturuki, ambako viongozi wa nchi 20 zenye uwezo mkubwa zaidi kiuchumi za G20 wanakutana, Bwana Juncker alisema watu waliohusika na ghasia ni wahalifu, wala siyo wakimbizi.
Image copyrightGetty
Image captionRais wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker
Mmoja wa washambuliaji, ametambulika kuwa ni raia wa Syria, ambaye aliingia Umoja wa Ulaya, kupitia Ugiriki, majuma sita yaliyopita kama mhamiaji mkimbizi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!