Na Emanuel Madafa,Mbeya
IDADI ya vifo vya watoto wachanga imeendelea kupungua
Mkoani mbeya kutoka vifo 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568 kwa mwaka
2014 ambapo ni sawa na asilimia 5.7.
Hali hiyo inatokana timu ya uendeshaji wa huduma za afya
mkoa kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kuweka maazimio ambayo
wamekuwa wakiyatekeleza kwa pamoja.
Akizungumza jijini Mbeya mratibu wa huduma za afya ya
uzazi na mtoto mkoani humo Ndugu Prisca
Butuyuyu amesema kutokana na
usimamizi huo wameweza kufuatilia mambo
mbalimbali yakiwemo ya upatikanaji wa dawa .
Amesema hatua nyingine iliyofanikisha zoezi hilo ni
pamoja na kushughulikia mapungufu na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza
katika vituo vya huduma.
Amesema sanjali na
mafanikio hayo pia wanatoa pongezi za dhati kwa shirika la UNICEF kwa kuendelea kusaidia kutoa fedha za
usimamizi shirikishi katika eneo la
huduma za afya na uzazi na mtoto.
Butuyuyu amesema kuwa baadhi ya halimashauri zimeweza kuendesha semina mbalimbali kuhusu uzazi salama ambazo ni
huduma baada ya kujifungua pamoja na
huduma muhimu kwa watoto wachanga.
Hata hivyo amesema
shirika la UNICEF wakishirikiana na KOICA
wamekuja na mpango mwingine wa miaka 4 ya uboreshaji huduma za afya ya
uzazi na mtoto.
Mwisho
JAMIIMOJABLOG
No comments:
Post a Comment