Wednesday, 18 November 2015
HESLB imetoa majina ya awamu ya 4 kwa wanafunzi ya walioomba mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE NA YA MWISHO yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote nne yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Mwisho.
CHANZO: JMF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment