Monday, 9 November 2015

AINA ZA MAZIWA YA KOPO (BABY FORMULA) NA MATUMIZI YAKE


 Maziwa ya kopo (baby formula) ni maziwa ya ngo'mbe wana ya process na kuweka kwenye mfumo wa powder,na kuongezea virutubisho vingine.

Maziwa ya kopo  yana utofauti sana na maziwa ya mama sababu maziwa ya mama yanavirutubisho vingi  ni asilia vinavyo mpa mtoto kinga mwilini na kumwongezea uzito mtoto kwa haraka ,wakati maziwa ya kopo yanachukua mda kumkuza mtoto na kumpa kinga ndogo mwilini na kumfunga choo.



sababu zitakazo pelekea mtoto kupewa maziwa ya kopo?


  • Mama kutokuwa na maziwa ya kutosha

  • Mtoto kutokushiba maziwa ya mama(hayamtoshi)

  • Mama kupatwa dharura (kupata safari ya mda mrefu,kuumwa au kifo n.k)

Wazazi wengi wanakosea  kuwapa watoto maziwa ya kopo kusipo sababu maalum,mtoto anatakiwa apewe maziwa ya kobo iwapo kuna sababu malum na ushauriane na daktari, lasivyo ni vizuri mtoto anyonyeshwe  maziwa ya mama ili apate virutubisho na kinga mwilini vitakavyo mwepusha na maradhi.



Aina za maziwa ya kopo 


Kuna aina nyingi za maziwa ya kopo ya watoto ,kuna mengine yalishapigwa marufuku nchini Tanzania kama (lactogen n.k)ila kuna baadhi yanatumika na ni mazuri kama

:Nan,

:Sma kopo la gold

:S26 köpö la gold

:Baby infant

:Cow gates


MADHARA YA MAZIWA YA KOPO


Maziwa ya kopo ni hatari sana kwa watoto sababu uaminifu ni mdogo ,kwa mfano Tanzania wafanya biashara wengi sio waaminifu  wanauza maziwa fake kwa kujali maslai yao na selikali inatoa onyo mara kwa mara,mzazi unatakiwa kuwa makini sana maziwa fake huadhiri ini,figo ,kuhara,kutapika,kupata rashes,maumivu ya tumbo au kupata cancer .



USHAURI TOKA AFYA BORA KWA MTOTO


1:Maziwa ya kobo ukifungua kutumia unatakiwa utumie kwa siku 30 zaidi  hapo hayafai tena kutumika mwaga.


2:Chemsha maji ya kutengenezea maziwa kabla hujachanganya na maziwa.


3:Hifadhi maziwa kwenye chombo cha plastic chenye mfuniko hakikisha hewa haipiti,kopo la maziwa yenye material ya steel(bati) ni sumu mbaya huchochea kupata cancer kwa urahisi.



107908280
MAZIWA YALIO HIFADHIWA KWENYE CHOMBO CHA PLASTIC

4:Unachotakiwa nunua maziwa yalio pakiwa kwenye makopo ya plastic  au box dogo hayo ni mazuri zaidi  kama cow gate,sma haya yatatoka Uk.


5:Soma expiry date(siku ya mwisho maziwa kutumika) ni hatari sana,usimpe mtoto bila kusoma tarehe.


6:Yakague maziwa kwa kuweka kwenye chombo cha plastic mara nyingine yanakuja na uchafu ndani mende,pini n.k


7:Maziwa mengine huwa yanakataa watoto wanapata maumivu ya tumbo wengine hutapika hivyo unaweza mbadilishia.


8:Nawa mikono yako kwa maji safi kabla hujamtengenezea maziwa mtoto


9:Maziwa ya mama ni muhimu kuliko ya kopo au ng'ombe mtoto  anakuwa na kinga kubwa mwilini yako ni salama zaidi kwa afya yake.


KWA HISANI YA AFYA YA MTOTO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!