Thursday, 8 October 2015

ZIARA YA MAGUFULI VUNJO-LYATONGA MREMA AUNGANA NA CCM KWENYE KAMPENI AMUOMBEA KURA MAGUFULI.

Name:  M1.png
Views: 7790
Size:  324.5 KB
Mrema ametangaza kumuunga mkono mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli ingawa chama chake (yeye akiwa Mwenyekiti), TLP kina mgombea Urais pia.



Leo katika mkutano wa CCM katika jimbo la vunjo, akihutubia nyomi ya watu, mgombea urais wa CCM John Pombe Magufuli alimwombea kura mgombea wa TLP, Augustino Mrema kwa wakazi wa Vunjo kwamba wamchague kuwa mbunge wao huku mgombea wa CCM wa jimbo hilo Innocent Shirima akiwa pembeni yake akishangaa bila kuamini. 


Magufuli alisema pia kwamba mrema akichaguliwa atamwingiza kwenye baraza lake ya mawaziri.

Wakati hayo yakijiri viwanja vya himo, Mrema alikuwa njia panda na wakati Magufuli amemaliza mkutano wake alipita na 'entourage' yake kuelekea Same. 

Mrema alikuwa amesimama anaongea na watu hapo njia panda, msafara wa Magufuli ulimpita Mrema kuelekea Same, lakini baada ya dakika 10 convoy ya Magufuli ilirudi njia panda ili kumsalimia mrema, wakazi wa Vunjo walifurika na Magufuli alimwomba Mrema aongee kidogo. Mrema alimsifia Magufuli kwa barabara alizojenga katika jimbo la Vunjo. 

Magufuli nae alirudia akisema mbatia hafai kuwa mbunge ila wamchague Mrema ambaye ni jembe na mchapakazi kama yeye na watu walilipuka kwa shagwe
.

2 comments:

Anonymous said...

aziz bilalOct 9, 2015


1
Reply

Huyo hana lolote zaidi mbuzi ndio imempelekea kujifanya eti naye anamsuaka aka ya kujibeza ili apatiwe kula ,ni tamaa ya madaraka tuu ,mnafiki mkubwa huyo.

Anonymous said...

Musa nyakati20:39+1
0
1
1
Reply

namuomba mungu2 aiokoe tanzania katk kipnd hiki cha mpito

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!