Na Mwandishi Wetu, Katuma Blog tz.
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuhakikisha hawatangazi matokeo ya uchaguzi katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura bila idhini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Aidha, wametakiwa kutumia nafasi zao kuzuia machafuko kwa kuandika habari kwa kufuata miiko ya taaluma na fani ya uandishi wa habari na kuwaondoa hofu wananchi ya kuibuka kwa machafuko kupitia kalamu zao.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali.
Alisema siku zote waandishi wa habari wanapotumia vibaya kalamu zao kwa kuandika habari za uchochezi ndio huwa chanzo cha machafuko.
"Tunapaswa kupima kauli za wanasiasa kabla ya kuzichapisha au kutangaza, tuongozwe n amisingi ya utaifa katika kila jambo tunalofanya na pia kuwaelimisha wananchi kufuata sharia wakati wa kupiga kura na kutangaza matokweo," alisema Mwambene.
Alisema viasharia vya uvunjifu wa amani ni pamoja na kauli za baadhi ya viongozi wa siasa, wanaharakati, baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kauli za baadhi ya watafiti, viongozi wa dini na watabiri.
Aliwata waandishi kutoegemea upande wowote wa chama au mgombea, kutoa taarifa linganifu sambamba na kuwasiliana na vyanzo sahihi vya habari kabla ya kutoa habari hizo kwa jamii.
No comments:
Post a Comment