Baadhi ya wadau wa Vijana wakiwa katika maandamano kuelekea katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma ambapo hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana ilifanyika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akihutubia wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa jana mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa akihutubia wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa jana mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa (kushoto) akipeana mkono na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Msham Abdalla Khamis, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga.
Mwakilishi kutoka Asasi ya Vijana wa Afika Mashariki Tanzania (EAC YOUTH TZ) Bi. Mary Daniel akisoma risala kwa niaba ya Vijana wote wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa jana mkoani Dodoma. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Asasi ya Muungano wa Dini Bw. Roggers Fungo.
Mwakilishi kutoka Asasi ya Vijana wa Afika Mashariki Tanzania (EAC YOUTH TZ) Bi. Mary Daniel akikabidhi risala kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuuwa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa jana mkoani Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia ongezeko la Idadi ya watu (UNFPA) Bi. Tausi Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga mara baada kutoa salama za shirika hilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa jana mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Msham Abdalla Khamis,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa akifurahia mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa jana mjini Dodoma.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi (wa pili kutoka kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa (mwenye vazi la kitenge) akishauri jambo alipotembelea banda la UNFPA mara baada ya uzinduzi wa maadhimsho ya Wiki ya Vijana jana mjini Dodoma. Kushotoni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa (mwenye vazi la kitenge) akiangalia baadhi ya Filamu zilizokaguliwa na Bodi ya Filamu nchini alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya uzinduzi wa maadhimsho ya Wiki ya Vijana jana mjini Dodoma. Wapili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, na kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Picha na: Frank Shija, WHVUM
……………………………………………………………….
Vijana nchini wameshauriwa kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura na kuchagua viongozi wazalendo wapenda amani na watakaoleta maendeleo ya taifa kwa ujumla ifikia oktoba 25 mwaka
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Galawa jana mjini Dodoma wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani humo.
Galawa alisema kuwa Vijana wanapaswa kutambua wajibu wao kama raia na si kukubali kutumiwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi na kusisitiza kuwa vijana wajitambue na kuwa wazalendo kwa taifa lao.
“Vijana nyiemkifanya uamuzi sahihi tutapa viongozi waadilifu,wapenda amani na watakaotuletea maendeleo msikubali kurubuniwa.” Alisema Galawa.
Aidha Galawa alisema kuwa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo katika taifa kwa kuwa imekuwa ikiwakutanisha vijana mbalimbali na kubadilishana uzoefu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga alisema kuwa Serikali ilianzisha maadhimisho haya kwa lengo la kuenzi fikra za Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerer ambaye alikuwa anathamini sana mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa.
Aliongeza kuwa katika maadhimisho haya yamekuwa yakiambatana na shughuli mbalimbali zinazohusu vijana zikiwemo maonyesho ya vijana wajasiriamali, midahalo ya vijana, upimaji wa afya kwa hiari, michezo ya kuimarisha afya na upandaji miti.
Sihaba alitumia fursa hiyo kuwahimiza vijana kote nchini kujitokeza kwa wingi katika tarehe ya upigaji kura ili waweze kutumia haki yao ya kidemokrasia katika kuchagua viongozi watakao leta maendeleo ya taifa na kuacha nchi ikiwa na amani na utulivu.
Wakati huo huo katika risala ya vijana nchini iliyosomwa na Mwakilishi wao kutoka Shirika la Vijana wa Afrika Mashariki Tanzania Bi. Mary Daniel wameshauriwa kuwa makini hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kutokubali kurubuniwa kwa maneno ya chuki na kuhatarisha amani.
Katika risala hiyo vijana wameshauriwa kutambua kuwa uchaguzi ni tukio la siku moja tu hivyo kila mmoja atumie busara akitambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi na kuwataka vijana wote kuwa mawakala wa umoja wa kitaifa katika kudumisha amani na mshikamano uliopo.
Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yameanzishwa mwaka 2000 mkoani Kilimanjaro ambapo yamekuwa na kauli mbiu toafuti kulingana na wakati na matukio kwa mwaka huu maadhimisho haya yamekuja na kauli mbiu “Tumia haki yako ya Kidemokrasia kupiga kura tarehe 25 Oktoba 2015”

No comments:
Post a Comment