Saturday, 24 October 2015

MREMBO APELEKWA MAKABURINI AUAWA

Hilda Mwita enzi za uhai wake.
Chande AbdalLah na Gabriel Ng’osha
MAJONZI! Mrembo mmoja aliyefahamika kwa jina la Hilda Mwita (29) mkazi wa Kisanga, Bunju A jijini Dar, anadaiwa kupelekwa eneo la makaburini, ambako alibakwa hadi kufa, Risasi Jumamosi lina kisa kizima.

Tukio hilo la kuhuzunisha, lilitokea hivi karibuni, baada ya marehemu, aliyejulikana pia kama mama Papaa, kutoonekana nyumbani kwake kwa zaidi ya wiki nzima.
Akizungumza na Risasi Jumamosi mdogo wa marehemu, Grace Mwita (15) alisema siku ya tukio dada yake alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na baada ya muda mfupi, mwanaume mmoja ambaye hamfahamu kwa jina wala sura, alifika na kuzungumza kidogo na dada yake kabla ya kuondoka wote.
“Kabla ya kuondoka, dada aliniachia shilingi elfu ishirini na simu zake, tangu siku hiyo sikumuona tena hadi alipokutwa amekufa eneo la makaburi karibu na nyumbani,” alisema msichana huyo.
Inadaiwa kuwa siku tatu baada ya marehemu kuondoka, mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili, alilia kwa ajili ya kutaka kunyonya, kitendo kilichowashtua majirani waliomhoji Grace alipo dada yake, naye kuwaambia haelewi alipokwenda.
Mjumbe wa Shina la Kisanga, Boniface Maiga alisema mvua kidogo iliyonyesha maeneo hayo ilisaidia kugundulika kwa mwili huo, kwani baada ya kuacha, majirani walianza kulalamikia harufu kali iliyotokea eneo la makaburini.
“Mmoja wa majirani akaamua kwenda kuchoma takataka zilizokuwa eneo hilo, ndipo akaona mwili ukiwa umelala chali, hauna nguo hata moja.”
Ingawa taarifa za kipolisi na daktari bado hazijatoka, lakini mashuhuda wamedai marehemu alibakwa na muuaji au wauaji kabla ya kuuawa.
Kutokana na mwili kuharibika, polisi walitoa kibali kwa familia na majirani kuuzika mwili wa marehemu jirani na alipouawa huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Marehemu ameacha watoto wawili wadogo; Lania Latifu (4) na Papaa (2). Amezikwa Jumatano kwenye makaburi ya ukoo mwingine kutokana na mwili wake kuharibika vibaya.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!