Monday 26 October 2015

MOJA KWA MOJA:KUHESABIWA KWA KURA TANZANIA

10.56am:Kuna hali ya wasiwasi mjini Mwanza huku maafisa wa polisi wakikabiliana na vijana wanaodaiwa kutoka katika chama cha UKAWA.kuna visa ambapo vikosi vya usalama vilirusha gesi za kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.
Image captionZanzibar washeherekea
10.46am:Mda mfupi baada ya kumsikia Maalim Seif akiwaambia waandishi habari kwamba ameshinda raia walianza kusheherekea.


10.45am:Maalim Seif anasema kuwa amejipatia kura 277,000 huku mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha CCM akijipatia kura 178,363
10.44am:Mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais kisiwani Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad wa CUF amejitangaza mshindi kabla ya matokeo rasmi kutangazwa na tume ya uchaguzi kisiwani humo.
Anasema kuwa anajua mipango ya tume hiyo ya kutaka kubadilisha matokeo hayo.
Amesema kuwa CUF ina takwimu zinazoonyesha kwamba chama hicho kinaongoza katika vituo vya kupigia kura vya Unguja na Pemba,hivyobasi tume hiyo isifikirie kubadilisha matokeo hayo.
Image captionMwanza
10.24am:Hali ya kawaida imeanza kurudi mjini Mwanza huku biashara zikifunguliwa.Maduka yalikuwa mahame huku kile kilichojulikana kama mji uliokuwa na harakati nyingi ukibadilika na kuwa mahame.
10.19am:Tume ya uchaguzi imeanza kutangaza rasmi mateokeo ya urais katika jumba la mikutano la Julius Nyerere mjini Dar es Salaam
Image captionMaafisa wa usalama huko Mwanza
10.15am:Ulinzi mkali umewekwa kote nchini Tanzania huku tume ya uchaguzi ya taifa hilo ikianza kutoa matokeo ya uchaguzi.
Image captionVijana wailalamikia tume ya uchaguzi
9.35am:Hawa ni baadhi ya vijana walioajiriwa na tume ya uchaguzi kufanya kazi kadhaa wakati wa uchaguzi katika eneo la Mwanza .Wameishtumu tume ya uchaguzi kwa kuwanyima marupurupu yao.
Image captionKImara raia wanapiga kura
9.28am:Wazee na walemavu ndio watu walioathirika zaidi na tataizo hilo kwa kuwa iliwabidi wangojee tena.Hatahivyo wamewasili katika kituo hicho.
Image captionKimara
8.45am:Hatimaye wakaazi wa eneo la Kimara Stop Over mjini Dar es Salaam wameanza kupiga kura baada ya shughuli hiyo kukwama siku ya jumapili baada ya maafisa wanaosimamia shughuli hiyo kutofautiana na wale wa tume ya uchaguzi na hivyobasi kuchoma vifaa vya kupigia kura.
Image captionEneo la kimari raia hawakupiga kura siku ya jumapili
7:20am: Usalama umeimarishwa katika kituo kikuu cha kujumlisha matokeo katika ukumbi wa Julius Nyerere. Tume inatarajiwa kutoa matokeo ya kwanza saa tatu.
Image captionMasanduku ya kupigia kura
7:15 am: Mjini Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania, masanduku ya kura yanaendelea kukusanywa katika afisi kuu kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuhesabu kura.
Image captionUchaguzi tanzania
7.00 am: Maafisa wanaanza kuingia mmoja mmoja kituo cha kupigia kura Kimara Stop Over, Dar es Salaam ambako wapiga kura wanatarajiwa kupiga kura zao za urais na ubunge baada ya uchaguzi kutatizika siku ya jumapili. Wapiga kura walifikia kituoni tena mapema sana leo.
Image captionRaia wa kwanza
6.00 am: Kituo cha Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam ambako uchaguzi unafaa kufanyika leo baada ya kutatizika jana, maafisa wa kusimamia uchaguzi bado hawajafika kituoni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imesema itaanza kutoa matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais leo saa tatu katika jumba la mikutano la Julius Nyerere, Dar es Salaam. Hata hivyo kuna maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika Jumapili.
ASUBUHI NJEMA RAIA WA TANZANIA

CHANZO:BBC SWAHILI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!