Saturday, 24 October 2015

MOI WAOMBWA KIMPELEKA MGONJWA KUPIGA KURA



Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi.

Dar es Salaam. Mkazi wa Jiji la Dar es Salaama, Chacha Makenge (38) ameuomba uongozi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa ya Muhimbili (MOI) msaada wa gari la wagonjwa kwa ajili ya kumpeleka kwenda kupiga kura katika Kituo cha Chuo Kikuu Dar es Salaam kesho.


Makenge amelazwa wodi 17 Sewahaji iliyopo MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN), akipatiwa matibabu baada ya kuvunjika uti wa mgongo na kusababisha kushindwa kutembea.
Ombi hilo limo kwenye barua aliyouandikia uongozi huo na nakala kupelekwa kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Serikali za Mitaa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makenge aliyeripotiwa awali kuishi kwenye handaki eneo la Chuo Kikuu Dar es Salaam, amelazwa wodini hapo baada ya kupata ajali na kuvunjika mgongo.
“Mimi ni mgonjwa nimelazwa tangu Septemba 8 mwaka huu, wodi namba 17 Sewahaji nimasumbuliwa baada ya kuvunjika, nahitaji gari la wagonjwa linipeleke kituo cha kupigia na kunirudisha hospitali kuendelea na matibabu,” alisema na kuongeza kuwa anatambua kupiga kura ni haki yake kikatiba.
Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi alithibitisha kupokea barua ya mgonjwa huyo na uongozi wa taasisi hiyo kushughulikia ombi hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Mpigakura na Habari wa NEC, Clerence Nanyaro alisema hakuna utaratibu wa kumpeleka mtu au kikundi kwenda kituoni kupiga kura bali ni jukumu la ndugu

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!