Saturday, 3 October 2015

MLIPUKO WA BOMU YAUA WATU 15 NIGERIA

Image captionHasara inayosababishwa na milipuko ya mabomu nchini Nigeria
Milipuko miwili ya mabomu ambayo ilikumba maeneo ya viungani mwa mji mkuu wa Nigeria Abuja yamewaua watu 15 na kuwajeruhi wengi kulingana na maafisa.


Mlipuko wa kwanza ulikumba kituo kimoja huko Kuje yapata kilomita 40 kutoka mji wa Abuja.
Mlipuko wa pili ulikumba kituo cha mabasi huko Nyanya.
Hakuna kundi lililosema lilitekeleza shambulizi hilo lakini kundi la Boko Haramu linatuhumiwa kutekeleza mashambulizi hayo.
Huku kundi hilo likihusishwa na mashambulizi mjini Abuja hapo awali,wapiganaji wake wamelenga sana maeneo ya Kaskazini mashariki.
Maiduguri,ambao ndio mji mkuu wa jimbo la Borno ndio eneo ambalo wapiganaji hao walianzisha kampeni zao kwa lengo la kubuni taifa la kiislamu mwaka 2009.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!