Anasema kamati kuu haiwezi kusema watu watano au sita ni hawa bila kuwasikiliza, kilichotokea mwaka huu ni tofauti kabisa kilichotokea mwaka 1995, safari mwenyekiti ni Jakaya Kikwete, kilichotokea ni jambo kubwa katika historia yetu na mimi katika historia yangu pale ambapo naona kwamba katiba inavunjwa nimekuwa na tabia ya kusema waziwazi na kuwaambia wenzangu si sawa.
Mwaka 1972 nikiwa mkuu wa mkoa Simiyu, kulikuwa na Bunge Dar es Salaam, nikakuta kuna mswada wa kurekebisha katika kuhusiana na swala la wakuu wa mikoa. Mchango wangu uliibua hisia kali na kumwambia mwenyekiti muswada aurudishe maana hatuukubali, kwa upande wa watu walipo serikalini walisema ndio na wabunge wa kuchaguliwa walisema hapana.
Ilipofika zamu yangu nikasema sina upande, wabunge walifurahi sana. Kura zilipohesabiwa serikali ilishindwa kwa mara ya kwanza katika mfumo wa serikali ya chama kimoja. Mzee Kawawa aliniita akasema wewe ni mwenzetu lakini umetuacha, Rais atakubadilisha kazi.
Nilipoitwa na mwalimu nilimueleza kwa nini nilikataa na akasema ningekuwa katika nafasi yako ningepinga lakini mimi ndio naongoza nchi lakini usiwe na wasiwasi. Tukakubaliana na siku ya pili nikatangazwa nimeachishwa uwaziri. Nilifanya uamuzi ule nikijua kabisa naweza kupoteza kazi lakini kwenye masula ya kimsingi huwa sitetereki.
Mimi sikubaliani na mambo yaliyotokea tarehe kumi na kumi na moja Dodoma, kilichotokea ni kuwadhalilisha wagombea wenye haki, kamati kuu ingeweza kuwahoji na kuamua. Hili halikfanyika. wadhalilishwa, wamezungushwa mikoa 15 kwa gharama zao na kuishia mlangoni mwa kamati kuu.
CCM inaamini binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshma ya kutambuliwa utu wake, kuwazungusha alafu nyinyi mmefunga mlango, si kuwadhalilisha? Katika nchi yetu hao waliodhalilishwa wamenyamaza moja kwa moja isipokuwa Mwandosya, aliinuka na kusema kwamba kweli wamedhalilishwa na kadhalika.
Nawapongeza Kimbisa, Sophia na Nchimbi kwa kueleza yaliyotokea kamati kuu, tuliingia chama hiki si kwa ajili ya kutafuta cheo na wengine tuliacha kazi kwa mkoloni. Tulitafuta chombo cha ukombozi kwa watanzania na waafrika.
Kwa kuwa uongozi wa sasa wa chama cha mapinduzi kufanya yale wanayotaka wao kwa maslahi ambayo sina hakika ni ya nani, vijana wanatumiwa kudhalilisha watu wazima, watu wanaajiriwa kutukana tu watu, mimi nasema sikubaliani na hiko sio chama tulichoshirikiana kukijenga.
Mimi kuanzia leo naachana na chama cha mapinduzi kwa sababu siwezi kuhimili chama kinachoendeshwa bila kuheshimu katiba kwa sababu katiba ndio inayotuunganisha sisi sote. Sasa nasema kuanzia sasa najitoa chama cha mapinduzi, najua uamuzi wangu utasumbua baadhi ya rafiki zangu, makada wenzangu na wazee wenzangu hata vijana lakini ni uamuzi ambao lazima niufanye kwa sababu vinginevyo mimi nitajisaliti mwenyewe.
Nimehusika kuweka misingi ya chama chetu, ndani ya chama chetu kumekuwa na demokrasia halafu wakuu wanakwenda kutangaza kwenye majukwaa hakukuwa na tatizo lolote, mambo yote yalikuwa sawasawa.
Sikusudii kujiunga na chama kingine chochote na nina sababu, mimi nimekuwa mwanaharakati wa TANU na CCM kwa muda wa miaka 61, nadhani miaka 61 inatosha mimi kuwa mwanaharakati.
Tatu mimi ni raia tena raia huru wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, nna haki zangu za kisisasa na kijamii hivyo nitaendelea misimamo yangu.
Katika hali ya sasa ina makundi mawili, moja linasema kidumu chama tawala maana yake hakuna mabadiliko. Kundi jingine linasema linataka mabadiliko katika nchi yetu, sitaki kusema kundi lipi kubwa lakini nasema hali iko hivyo, kwa jinsi nnavyotazama vijana wanataka mabadiliko ukiondoa vijana wangu wa UVCCM, kina mama walio wengi wanataka mabadiliko, wafanyakazi wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimba migodi wadogowadogo najua wengi wao wanataka mabadiliko, wanafunzi hasa wa sekondari ya juu, wa vyuo na vyo vikuu na wasomi wa nchii walio wengi wanataka mabadiliko.
Nilisema siku moja nilipoulizwa nani unamuona anafaa kugombea Urais, niliwaambia kwamba mimi nitamuunga mkono yule ambae ziko dalili zote wananchi wanasema ndie anaefaa. Pia nilisema nilipokuwa na ndugu Lowassa Arusha, Mwalimu alisema ulizeni wananchi wanasema nini?
CHANZO JAMII FORUM
1 comment:
aziz bilal18:37
1
H pia ni corrupt uyu mzee ni mnafiki mkubwa sana .
Post a Comment