Mgombea urais kupitia chama cha Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa amesema watanzania wakimpa ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha anadhibiti vifo vya mama na mtoto.
Majira ya saa nane mchana akiwa kwenye jukwaa la kampeni mjini Moshi.
Sauti ileile pia ilisikika majira ya saa tano asubihi alipowasili Tarakea mjini Rombo.
Edwrad Lowassa anayetamba kama mkombozi wa Tanzania ijayo, amesema kama watanzania watampa ridhaa ya kuwa rais atahakikisha anadhibiti vifo vya mama na mtoto hapa nchini.
Akiwa mjini Tarakea mpakani mwa Tanzania na Kenya akatumia jukwaa hilo kutangaza neema kwa watanzania waishio mipakani
Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema taifa anasema nafasi hii ni muhimu kwa watanzania kuitumia kwa kukiondosha madarakani chama cha CCM kwani licha ya kushindwa kuleta mabadiliko bali pia kimechoka na hakipaswi kuendelea kuwepo madarkani.
Akiwa mjini Kilimanjaro Edwrad Lowassa usafiri wa chopa ulimrahisishia kazi kwa kufanya mikutano katika majimbo ya Rombo, Moshi mjini, Siha na Karatu ambapo comledy Kingunge Ng’ombale Mwiru akatoa neno kwa watanzania.
No comments:
Post a Comment