Mahakama kuu ya rufaa nchini Afrika Kusini imedumisha hukumu aliyopewa mfalme wa kabila la Nelson Mandela la Thembu, ikisema lazima atumikie kifungo cha miaka 12 jela.
Mfalme Buyelekhaya Dalindyebo alikuwa amepatikana na hatia ya kushambulia watu, kuteketeza mali, kuteka nyara watu na kujaribu kuzuia utekelezaji wa haki.
Mfalme huyo alikuwa amewaadhibu baadhi ya watu wake kwa kuteketeza nyumba zao, kuwapiga na kuteka nyara familia ya mwanamume mmoja.
Dalindyebo alihama chama tawala cha ANC na kujiunga na chama cha upinzani cha DA 2013
Kiongozi huyo anatakiwa kujiwasilisha gerezani katika muda was aa 48 zijazo.
Rufaa yake ilianza 2009, alipohukumiwa kifungo cha miaka 15 na mahakama kuu katika mkoa wa Eastern Cape.
Mfalme huyo anakumbukwa kwa kukataa kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela mwaka 2013.
Hii ni baada yake kujibizana na Rais Jacob Zuma, ambaye alimuita “Mvulana wa Kizulu”. Wakati mmoja pia alisema angeacha kuvuta bangi tu iwapo Bw Zuma angeacha kuwa mfisadi.
Lakini baadaye aliomba radhi kwa rais na hata kumkabidhi ng’ombe.
No comments:
Post a Comment