Thursday, 22 October 2015
MAMBO UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU KIFAFA('EPILEPSY':)
Mtu anaanguka chini na kupoteza fahamu,mwili wake unakakamaa kisha unaanza kusukasuka,mmoja kwa mmoja hiyo ni kifafa.
Kifafa ni ugonjwa unaothiri utendaji wa ubongo na kukata mawasiliano kati ya mwili,mtandao wa ubongo na uti wa mgongo
unaomfanya mtu azimie,apoteze fahamu na asijitambue kabisa kwa dakika tano au zaidi kutokana na ukubwa wa tatizo
Endapo kuzirai kumekaa zaidi ya dakika tano japo ni nadra huwa ni hatari sana nani lazima huduma ya haraka itafutwe hospitalini kuokoa maisha ya mhanga.Mhanga anapozimia katu usithubutu kumzuia kwa kutumia nguvu kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia anayejaribu kumsaidia,kusukasuka au kujinyonga kunapoanza kupungua hakikisha ya kwamba kupumua kumerudia hali ya kawaida. Mhanga anapozimia,weka kitu laini kati ya kichwa chake na sakafu na uondoe vitu vyote vyenye ncha kali vilivyo karibu na kichwa chake,mwili unapoacha kusukasuka,mgeuze alalie ubavu wake kama picha unavyoonyesha
Mhanga anapopata fahamu kwanza mhakikishie kwamba yupo salama,kisha msaidie asimame wima na umwongoze hadi mahali anapoweza kupumzika kabisa kwani wahanga wengi huwa wanachanganyikiwa na wanahisi usingizi baada ya kuzimia,wengine hupata nafuu upesi na wanaweza kuendelea kufanya kazi walokuwa wakifanya kabla ya tukio hilo.
Sio wote wenye kifafa hukakamaa na kujisukasuka ila baadhi hupoteza fahamu kwa muda mfupi sana bila hata kuanguka chini,hatua hii ya kifafa huitwa'tonic phase'ambapo mgonjwa huwa haathiriki kwa muda mrefu na dalili zake kuu ni kutembea huku na huku ndani ya chumba,huvuta mavazi yake kwa nguvu au ahisi kizunguzungu. Wahanga wengi wa kifafa huwa na hofu ya kuanguka kila wakati kwa kuwa hawajui ugonjwa utawashika tena lini na utawashika wapi na hujihami kuwa mbali na watu kukwepa aibu ambalo ni kosa kubwa kwani endapo watapata mshtuko hukosa mtu wa kuwasaidia. USHAURI:tuwatie moyo,tuwe nao karibu,tuwasikilize kwa makini muda wote,wajipumzishe vya kutosha,wafanye mazoezi na wahudhurie clinic.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment