Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono viongozi na wanachama wa UWT wa Mkoa wa Mara wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre kwa ajili ya mkutano wa ndani na wanachama hao tarehe 3.10.2015.
Umati wa wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiongea nao Mjini Musoma tarehe 3.10.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Mkoa wa Mara wakati alipokutana nao kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre tarehe 3.10.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment