Wednesday, 7 October 2015

MAMA LULU ANGENIPELEKA JELA-MAMA KANUMBA




MAMA mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka kuwa endapo urafiki wao na mama Lulu, Lucresia Karugila ungeendelea, kuna siku angejikuta gerezani kwani angeweza kumfanyia kitu kibaya.


Akipiga stori na gazeti hili, Flora alisema anashukuru urafiki wao kusambaratika kwani mara nyingi kwenye maongezi yao, hasa akiwa amepata kiburudisho, mama Lulu alikuwa akiropoka maneno ya ajabu yenye kumkwaza na kumtia hasira.
“Yaani namshukuru Mungu alivyotukosanisha maana alikuwa akitoa maneno ya hovyo ya kunitia hasira, akidai mwanangu hakuwa na akili, eti mwanaye Lulu ndiye mwenye akili ndiyo maana hakaukiwi pesa, wakati mwingine akinitukana na kunikashifu bila sababu,” alisema mama Kanumba
Chanzo:GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!