Mgombea wa urais kupitia chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli amepiga kura asubuhi hii huko Chato.
Baada ya zoezi la kupiga kura, Dr Magufuli aliulizwa na waandishi wa habari iwapo atakubaliana na matokeo kama itatokea akashindwa.
Katika majibu yake, Magufuli amejibu kwa kifupi kuwa Tusubiri matokeo yatangazwe.
Aidha, Dr. Magufuli aliulizwa jinsi alivyojipanga kama itatokea akashinda ambapo pia alijibu kwa kifupi kuwa tusubiri tutajionea mara baada ya kuapishwa
No comments:
Post a Comment